March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

0-4064x3074-0-0#

Vijana Ilemela watakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi ndani ya halmashauri

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza

Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,mkoani Mwanza,wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo ndani ya halmashauri hiyo pamoja na kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

Hayo yamezungumzwa Agosti 26,2025,na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ally Ussi,wakati alipofunga kongamano la vijana la kujadili fursa za uchumi, uongozi,uadilifu,stadi za maisha na uzalendo kwa taifa,lililifanyika uwanja wa Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ally Ussi, akizungumza wakati akifungua kongamano la vijana la kujadili fursa za uchumi, uongozi,uadilifu,stadi za maisha na uzalendo kwa taifa,lililifanyika uwanja wa Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza

Ussi amewasisitiza vijana kuwa wabunifu na kujitokeza kuchangamkia fursa zinazotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ikiwemo mikopo ya asilimia 10 fedha za mapato ya ndani ambayo imeanzishwa mahususi kwa ajili yao.

“,Vijana baada ya kuunda vikundi tumieni mikopo ya asilimia 10 kuibua fursa za kiuchumi .Vijana wazalendo nimewaona Ilemela, waliopatiwa fedha sh. milioni 50, wameweka heshima kubwa na kumheshimisha Rais Dk.Samia ambaye yuko tayari kuona vijana wanakwenda kuibua fursa na kutumia fedha za mikopo kwa weledi,”amesema Ussi na kuongeza:

“Mwaka huu ni wa uchaguzi vijana mkashiriki kwa amani na kupiga kura, pia mkahamasishe wenzenu pamoja na familia ili wenye sifa wakashiriki kupiga kura na kutimiza haki yao ya kidemokrasia na kikatiba .

Awali Ofisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Asasi za Kiraia wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Yusuph Omollo, amesema fursa za kiuchumi kwa vijana zinazopatika katika Halmashauri hiyo zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni fursa za kifedha,kihuduma na kiuwekezaji.

Omollo amesema,fursa za kifedha zinazopatikana katika Halmashauri hiyo ni pamoja na mkopo wa asilimia 10, ambao utolewa kwa vikundi vilivyosajiliwa ikiwemo vikundi vya vijana asilimia 4, wanawake asilimia 4 na watu wenye ulemavu asilimia 2.Pia kuna fursa za kifedha zinazotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii kupitia benki ya NMB kwa mtu mmoja mmoja au kikundi.

Amesema fursa nyingine ni mkopo wa ufugaji na uchakataji wa samaki na vyombo vya uvuvi,unaotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Halmashauri kwa vikundi vya kijamii, kampuni,mashirika na mtu mmoja mmoja ambao wanakopesha vifaa ikiwemo vizimba vya ufugaji wa samaki ndani ya Ziwa Victoria.

“Fursa hii ipo kwa vijana,wapo vijana ambao wameisha fanya uwekezaji huo na kuanza kuona matunda.Hii yote ni kusaidia vijana katika suala la mitaji ili waweze kufanya uwekezaji na biashara pamoja na kuondokana na changamoto ya ajira,”.

Ofisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Asasi za Kiraia wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Yusuph Omollo

Omollo amesema,uwepo wa masoko rasmi 10,na kila Kata kuwa na masoko pamoja na yale madogo madogo ambayo hayajarasimishwa ndani ya halmashauri hiyo ni fursa ambayo vijana wanaweza kutumia kufanya biashara na kuchochea uchumi binafsi na taifa.

Pia amesema,uwepo wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 78.06,ambayo imegusa Kata 18 kati ya Kata 19,barabara ya changarawe yenye urefu wa Kilomita 125.53 na imepita katika Kata zote 19 za Halmashauri na mitaa 152 kati ya mitaa 171,ni fursa ya vijana kufanya biashara kwani maeneo yote yanafikika kwa urahisi.

Aidha amesema,nishati ya umeme imefika katika Kata zote huku huduma ya maji ikiwa imefika kwa asilimia 92, hivyo ni fursa ya vijana ambao wanaweza kutumia uwepo wa umeme na maji kubuni biashara na kujikomboa kiuchumi.

Vilevile amesema Halmashauri hiyo ina mialo 6 na fukwe hivyo vijana wanaweza kutumia fursa hizo kubuni biashara au kufanya uwekezaji na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Mchungaji Dkt.Jacob Mutashi akiwaslisha mada ya uongozi na uzalendo,

Sanjari na hayo Omollo amesema vijana wanaweza kutumia fursa ya uwepo wa Ziwa Victoria kujikomboa kiuchumi kwa kuanzisha boti za kitalii ndani ya Ziwa,usafiri wa boti na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba,kufanya shughuli za uvuvi pamoja na kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Mchungaji Dkt.Jacob Mutashi akiwaslisha mada ya uongozi na uzalendo,amesema wazazi wanapaswa kuwaeleza vijana historia ya taifa letu, mazuri ya maendeleo ili waelewe badala ya kuponda kila kitu, huku akiwataka vijana kuiga mfano wa Mwalimu Julius Nyerere , kwa uzalendo wa kuipenda nchi yake aliacha Ualimu ili kupambana na wakoloni.