December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vijana 400 kunufaika na mradi wa BBT

Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya

VIJANA 400 kati ya 129,000 Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ,wanatarajia kunufaika na mradi wa program ya kujenga kesho nzuri kwa vijana(BBT).

Mradi huo ambao unatarajia kuanza hivi karibuni baada ya serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuboresha miundombinu ya barabara na kusafisha mashamba.

Akizungumzia na TimesMajira Online katika maonesho ya wakulima nane nane kitaifa ambayo yanafanyika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya ,Mkuu wa Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Cuthbeth Mwinuka amesema tayari halmashauri imetenga eneo lenye ukubwa wa hekali 56,000 kwa ajili ya mradi huo.

“Program hii ni maalum kwa vijana na itakuwa tija kubwa na fursa kubwa ya kujiajiri na kuajiri wengine kwa kuzingatia mazao ya kimkakati ikiwepo ,soya,korosho na kuwa na uhakika wa chakula,”amesema.

Akizungumzia mradi huo, Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka amesema umekuja wakati mwafaka ambapo vijana wanauhitaji mkubwa wa ajira .

“Matarajio yangu kama mwakilishi wa wananchi, vijana wengi sasa wataondokana na changamoto ya ajira kwani eneo lenye ukubwa wa hekali 56,000 ni fursa kubwa kwa vijana kuwekeza kwenye kilimo,”amesema.

Masache amesema mbali na mradi huo wa BBT ,Serikali imetoa fedha zaidi ya bilioni 11 kwa ajili ya mradi wa maji kwa miji 28 na yote hiyo ni kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake.

Kwa upande wake ,Diwani Kata ya Itewe Wilaya ya Chunya ,Alex Kinyamagoha amesema kuwa mradi wa program ya kujenga kesho kwa vijana utaleta tija kwa vijana kujiajiri.