LONDON, England
KLABU ya Crystal Palace imethibitisha kumntakua aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira kama meneja wao mpya
ambaye atadumu hapo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Timu hiyo ilikuwa kwenye uwindaji wa bosi mpya tangu hapo
Roy Hodgson alipojitenga na klabu hiyo katika msimu wa joto baada ya timu kuwa katika mwendo wa kusuasua.
Akizungumza mara baada ya kuingia mkataba ba timu hiyo Vieira amesema, amefurahi sana kupewa nafasi hiyo ya kurejea tena England kusimamia mwenendo mzuri wa timu ili iweze kufanya vyema.
“Kuna mipango mingi ndani ya klabu hii ambayo imenivutia sana,
baada ya kuzungumza mengi na mwenyekiti na
mkurugenzi kuhusu matarajio yao na mipango yao kwa ujumla,” amesema Vieira.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania