Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
VIATU vya msanii maarufu wa Hip hop nchini Marekani Kanye West ‘Nike Air Yeezy 1’, ambavyo ndio vya kwanza kutengenezwa na msanii huyo, vimeuzwa kwa thamani ya kitita cha dola milioni 1.8, takribani TSh. Bilioni 4.1 kwenye mnada uliofanywa na kampuni ya Sotheby’s juzi.
Viatu hivyo, vinatajwa kuwa ndio viatu ghali zaidi kuwahi kuuzwa duniani kwa muda wote.vilivyonunuliwa na Kampuni ya RARES.
Thamani ya viatu hivyo imeivunja rekodi ya awali ya sneakers zinazouzwa kwa gharama kubwa iliyokuwa inashikiliwa na jozi ya viatu mwaka 1985, Nike Air Jordan 1s ambavyo viliuzwa mwaka jana kwa dola 615,000 zaidi ya TSh. Bilioni 1.4
Kanye alivaa viatu hivyo aina ya Nike Air Yeezy 1 kwa mara ya kwanza mwaka 2008 wakati akitumbuiza kwenye tuzo za Grammy.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA