Na Joyce Kasiki,Timwamajira online Mbeya

KATIBU Mkuu ,Ofisi ya Waziri Mkuu Mary Maganga ametembelea banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika maonyesho ya wiki ya Vijana mkoani Mbeya ambapo amejionea kazi mbalimbali zinayofanywa na vijana wakiwemo wenye ulemavu.
Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu huyo Balozi wa watu wenye mahitaji maalum wa VETA Francis Antony, amesema yeye ni muhitimu wa fani ya kompyuta katika chuo cha VETA ambayo yamemwezesha kuwa mwalimu wa wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma VETA.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha vijana wenye mahitaji maalum ili wasibaki nyuma katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
“Mimi ni mhitimu wa VETA na kwa sasa ni fundi wa kompyuta na mkufunzi mwenye ujuzi katika nyanja mbalimbali za ufundi. “Amesema Francis

Alisisitiza kuwa mafanikio yake ni ushahidi kuwa vijana wenye mahitaji maalum wana uwezo mkubwa wa kujifunza na kufundisha wenzao.
Naye Riziki Ndumba, mwanafunzi wa VETA Songea anayesomea fani ya ushonaji, alieleza kuwa alijiunga na mafunzo akiwa hana ujuzi wowote lakini alipokelewa vyema na walimu pamoja na uongozi wa chuo.
Riziki amesema amemaliza kozi ya miaka miwili na sasa anaamini anaweza kufanya kazi kama watu wengine, licha ya kuwa na ulemavu. Alitoa pongezi kwa VETA kwa kutambua uwezo wa watu wenye mahitaji maalum na kuwawezesha kwa vitendo.

Awali Afisa Habarinwa VETA Eimer Sarao, amesema VETA imekuwa mstari wa mbele kuwajengea uwezo walemavu ili kundi hilo nilibaki nyuma katika maendeleo yao na hivyo kuchangia katika Pato la Taifa.
Mafunzo haya ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA ni sehemu ya juhudi za serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha ushirikishwaji wa watu wenye mahitaji maalum katika maendeleo ya Taifa.
.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina