March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

VETA yaja na teknolojia mpya ya mafunzo uchomeleaji vyuma

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online

, CHUO cha Ufundi Stadi VETA Dodoma, kimeleta teknolojia mpya ya ‘simulation welding machine’ inayowezesha wanafunzi kufanya mazoezi ya uchomeleaji kwa ufanisi mkubwa bila kupoteza vifaa vya kufundishia..

Akizungumza Julai 8,2025 katika banda la VETA kwenye maonyesho ua Kimaitafa ya 49 yanayoendelea jijini Dar es Salaam ,Mkufunzi katika Chuo hicho fani ya kuchomelea Manfred Mapunda amesema,mashine hiyo inakwenda kuboresha ufundishaji katika fani hiyo .

 Mapunda, amesema mashine hiyo huwaruhusu wanafunzi kujifunza uchomeleaji kwa kurudia majaribio mara nyingi bila kutumia chuma halisi, jambo linalosaidia kupunguza gharama na upotevu wa vifaa.

“Awali tulikuwa tunatumia vifaa halisi moja kwa moja, lakini sasa mwanafunzi anaweza kurudia hadi mara kumi akiwa kwenye mashine hii, tofauti na zamani ambapo kila kosa lilimaanisha upotevu wa material,” alisema Mapunda.

Pia amesema , teknolojia hiyo inaruhusu kufundisha wanafunzi zaidi ya 50 kwa wakati mmoja kupitia mfumo wa projekta, hivyo kuboresha ufanisi wa mafunzo darasani. 

Kwa mujibu wa Mapunda Mashine hiyo pia imekuwa chachu ya kuongeza hamasa kwa vijana, hususan wasichana, kuingia katika fani ya uchomeleaji ambayo inatoa fursa nyingi za ajira na kujiajiri.

“Mashine hii ni rahisi hata katika ufudishaji ambapo mwalimu anaweza kumudu darasa lenye wanafunzi zaidi 50 tofauti na njia waliyoitumia awali ambayo mwalimu hulazimika kufundishwa wanafunzi 25 tu daradani,ndiyo maana tumeona tuje na hii mashine kuonesha vyuo vyetu vya VETA na wadau wengine wa tabia hii ya uchomeleaji ili nao waweze kuitumia katika ufundishaji na shughuli nyingine za kujipatia kipato.”alisema Mapunda

Kutokana na hali hiyo amesema,mashine hiyo inakuwa chachu ya kuongeza ufanisi wa wanafunzi wengi zaidi wanaohitaji kusoma fani hiyo wakiweka wanafunzi wa kike.

Aidha ametaja faida za fani ya uchomeleaji kuwa ji pamoja na kujiajiri kuajiriwa na kujipatia kipato na hivyo kuchangia katika Pato la Taifa.