January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

VETA yaja na mashine ya watoto Njiti

Na Penina Malundo,Timesmajira

MKURUGENZI wa kampuni ya Nyahende Medical Divices George Nyahende amesema mashine ya watoto wanaozaliwa bila kutimia miezi (njiti) ambayo imeifanyia ugunduzi ameitengeneza kwa teknolojia ya hali ya juu na kwamba ina uwezo wakufanya kazi hata katika maeneo ya vijiji.

Nyahende ambaye kitaaluma ni Mhandisi mitambo ametoa kauli hiyo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 48 yanayofanyika katika viwanja vya SabaSaba ambapo ni miongoni mwa waoneshaji bunifu waliopo katika banda Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadium (VETA)

“Kila hatua niliyokuwa naibuni nashirikisha wataalam ikiwemo madaktari,kulingana na maoni yao mashine yangu ni bora kuliko za nje,inafanya kazi katika mazingira yoyote,zile za nje kuna vitu hazina,mfano kwenye sehemu yakupumua unatakiwa ubonyeze madaktari wakaniambia huwa wanabonyeza mpaka wanalala mimi nikaweka mashine yakubonyeza automatically.

“Zile mashine za nje pia hazina sehemu yakupima uzito mimi mzani wa uzito kiasi kwamba mtoto akikaa hapa uzito wake unauona,pia nilikuta hospitali mtoto akiugua ugonjwa wa ngozi wanakimbizana kwenye mionzi,lakini kwenye mashine niliyoutengeneza mimi nikaweka mionzi,”amesema Mhandisi Nyahende.

Amesema mashinde hiyo ni rafiki zaidi na imekaa kitanzania na kwamba inaweza kufanya kazi katika mazingira yoyote kutokana na ukamilifu wake kwani hata ikipelekwa kijijini watalaam hawatadai mizani wala kifaa chakupimia mionzi.

Amesema kulingana na sheria iliyowekwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) tayari ameshafanya ulinganifu wa mashine hiyo na mashine zinazotengenezwa nchini Uingereza.“Nimesajili kiwanda na kibali chakuuza mashine hizi Tanzania na nje,naendelea kufanya uchunguzi mashine yangu,nimeshafanya ulinganishi na mashine zingine kama mamlaka inavyoelekeza,kwa hii nimeifanyia ulinganifu katika hospitali ya Serian na St.Elizabeth ambapo zikaonekana zipo sawa na za Uingereza anbazo wanatumia,”amesema Nyahende.

Amesema kutokana na ubunifu alionao endapo atapata usaidizi ana uwezo wakutengeneza mashine hizo za watoto njiti kumi kwa siku lakini endapo atakuwa anatengeneza mwenyewe ataweza kutengeneza moja kwa siku.Alisema ufumbuzi huo utausaidia serikali kuokoa fedha nyingi kwakuwa mashine moja ya kukuzia watoto ni Sh Milioni 80.