Na Penina Malundo, Timesmajira
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dar es Salaam imebuni Kifaa maalum cha kupimia uwezo wa kufundishia kwa watu wenye mahitaji maalum na kutambua uwezo wao kiurahisi wa kufikilia mambo mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,katika maonesho ya Biashara ya 47 ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere,Mwalimu wa Wanafunzi Maalum wa Chuo hicho ,Kintu Kilanga amesema kifaa hicho ni kirahisi kutambua uwezo wa mtoto mwenye ulemavu na kujua tatizo lipo wapi katika kuanza kumfundisha.
Amesema kifaa hicho ni maalum kwa kumfanyisha mtoto mazoezi na kujua wapi anatatizo na wao kuanza kumfundisha kwa urahisi.”Duniani kuna njia mbili ya kujifunza ipo ya kuonesha namna mtu anavyofanya na kujifunza na pia ipo ya uwezo wa kugundua kina cha uelewa,”amesema.
Amesema sababu kubwa ya kubuni kifaa hicho ni kutokana na kuona Jamii haitambui aina ya ulemavu ambao watoto wao wanao na kujua kuwa wanaaina moja ya ulemavu.
“Baadhi ya watu wanauelewa juu ya aina ya ulemavu ambao watoto wao wanao ambapo ujitoa na kuwapeleka vyuoni kujifunza vitu mbalimbali ikiwemo stadi za kazi ili kupata ujuzi ila wengi wao hawana uelewa wa aina ya ulemavu walionao watoto hao,”Amesisitiza
Kwa Upande wake Mwalimu Msaidizi wa Wanafunzi hao,Paulo anasema mwanafunzi mwenye uhitaji anapofika chuoni kwao upelekwa katika kifaa hicho na kupimwa uwezo wao na kujua namna ya kuanza kumfundisha.
Amesema kifaa hicho kinakuwa kinapima akili yake na ufahamu pamoja na kuona uwezo wao wa kufikilia.”tunaamini kuwa pale mtu anapofanya kazi fulani ndo anajifunza hivyo kifaa hiki kinamfanya mtoto mwenye ulemavu kujifunza vitu vingi,”amesema.
Aidha amesema hadi sasa kasi ya uandikishaji kwa Chuo chao ipo vizuri kwa kundi hilo kutokana na elimu wanayoendelea kuitoa katika maonesho hayo kila mwaka ambapo wamefikia wanafunzi 22 kwa Mwaka huu.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba