Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA),imebuni kifaa cha Maalumu cha kufukuzwa ndege shambani ambacho kinatumia sauti ya ndege aina ya Tai pamoja na umeme wa jua.
Lengo kifaa hicho ni kuwarahishia wakulima panapokuwa na ongezeko la ndege wengi waonaharibu mazao ya nafaka kuwafukuza.
Akizungumza katika Maonyesho ya ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) Mwalimu wa Umeme kutoka VETA Mikumi Jones Hokororo amesema wakulima wengi wanaolima mazao ya nafaka wamekuwa wakikumbana na chagamoto hiyo hivyo akaona ni bora kubuni kifaa hicho ambacho kitawatishia ndege hao wanaokula mazao.
Amesema kifaa hicho kinapokuwa shambani kinauwezo wa kulia kwa muda wa dakika 1 na kunyamaza kwa dakika 5.
” Mashine hii ya kufukuza ndege mashambani inauwezo wa kuhudumia hekari 5 pia kifaa hiki kinatumia umeme wa jua hata kukiwa hakuna jua kinauwezo wa kufanya kazi”amesema Hokororo
Hokororo amesema familia nyingi zimekuwa zikitumia muda mwingi mashambani kwa ajili ya kufukuza ndege wanaokula mazao kupitia kifaa hicho kitasaidia kuondokana na chagamoto hiyo.
“Kifaa hiki kinauwezo kutumika kulinda aina zote za mazao ya nafaka na kwamba kuanzia mkulima anapo panda mbegu zake mpaka mavuno”amesema
Aidha amewataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo ya kifaa hicho ambacho kinapunguza kundi kubwa la watu kwenda na badala yake kuendelea na majukumu mengine ya kujiongezea kipato kwa wanafamilia.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM