January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

VETA Mara wabuni kifaa cha kunyunyuza dawa shambani

*Ekari moja kutumia misunguko saba

Na Penina Malundo, TimesMajira Online

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA), wamebuni kifaa vya cha kunyunyuza dawa za magugu pamoja na kuua wadudu waharibifu wa mazao shambani.

Kifaa hicho zamani kilikuwa kikitumika kwa kubeba mgongoni kwa sasa unasukuma kama toroli ambapo kwa hekari moja unazunguka mara saba.

Katika mashindano ya ubunifu yaliyofanyika hivi karibuni, mashine hiyo ya kunyunyiza dawa ilishika nafasi ya pili hivyo inaonyesha kuwa suluhisho kwa wakulima.

Akizungumza katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Dar es Salaam, Mwalimu wa Chuo Cha VETA Mkoa wa Mara, Elly Nkonya amesema mashine hiyo imeongezewa uwezo ukilinganisha na ile ya kubeba mgongoni.

Amesema, uwezo wake ni mara 16 tofauti na kutokana na kuweka matundu 16 ambapo inamrahisishia mkulima kuweka dawa katika shamba kwa urahisi.

Amesema kuwa, wanabuni kifaa hicho kwa ajili ya kurahisisha shughuli za Kilimo kwani badala ya kuweka watu sita kwa ekari moja kwa kubebeshaajili ya kumwaga dawa, sasa mtu mmoja anaweza kufanya kazi hiyo.

“VETA kazi yetu ni kutatua changamoto kwa wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na kuweza kupata matokeo chanya kwa kutoa suluhu zana,” amesema Nkonya