Na David John
MKUU wa Chuo cha VETA Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera,Pascal Thomas amesema kuwa chuo hicho ni miongoni mwa vyuo vya Veta katika wilaya hiyo,ambapo Serikali ya awamu ya sita imeamua kuwekeza katika vyuo vya ufundi na kupanua huduma zake katika vyuo vya wilaya ambapo hapo awali kulikuwa na vyuo vya mkoa na vyuo ambavyo vilikuwa kwenye kanda.
Amesema kuwa wao karagwe wapo kanda ya ziwa ambayo inaunganisha mikoa ya Mwanza ,Mara ,kagera pamoja na Geita na katika mkoa wa kagera ambao una wilaya ya karagwe Misenyi ,kyerwa ,Ngara ,Muleba ,Biharamuro pamoja na Bukoba hivyo katika vyuo ambavyo vimepandishwa hadhi ni pamoja na chuo cha karagwe ambapo chuo hicho kihistoria kiliaza mwaka 1986 na kilikuwa kinamilikiwa na mtu binafsi ambaye alikuwa anaitwa Edmin MkendaKenda ambaye kwasasa ni Marehemu.
Thomas ameyasema haya leo Disemba 5 wilayani karagwe wakati akizungumza na waandishi wa Habari waliofika chuoni hapo. amefafanua kuwa baada ya aliyekuwa mmiliki wa chuo hicho kuona gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa ndipo aliamua kukabidhi kwa Halmashauri ya wilaya hiyo tangu mwaka 1992 na kuanzia mwaka huo chini ya Halmashauri ya wilaya kiliendelea kutoa huduma ya mafunzo ya ufundi nchini hivyo mpaka sasa hivi kinaendeshwa na Serikali kwa asilimia mia moja.
“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamna anavyowezesha Chuo cha Veta wilayani karagwe ,chuo cha Veta karagwe kinauwezo wa kuookea vijana 250 wa kwa kozi ndefu lakini hata kinazo kozi fupi fupi ambazo zinaendeshwa zaidi ya vijana 450 ambao tunaweza kuwapokea kwa mwaka hivyo uwezo wake hadi hivi sasa ukiweka kozi ndefu na fupi inamaana karibu vijana 700 wanaoweza kupokelewa na mpaka sasa tunao vijana 250 ambao wanategemea kufanya mtihani wa taifa ambao wa mwaka wa kwanza na mwaka wa pili.”amesema
Thomas amesema kuwa wanashuuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kuwa F⁶adhili vija na wasio nauwezo wapatao 109 ambao wanafadhiliwa kusoma kwa kozi ya miezi 6 na sasa hivi wanakwenda kuhitimu kozi hiyo vijana hao wamekuwa wakiwafundisha kwa muda wa jioni hivyo mpaka sasa hivi wanakwenda kuhitimu.
Amesema Serikali imeweza kutoa shilingi bilioni 4.6 71 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa chuo hicho na pia ameweza kutoa shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kununua vifaa na mitambo katika kalakana hivyo sasa hivi kalakana zimekamilika kwa asilimia kubwa.
Kwaupande mwanafunzi wa chuo hicho David Adam ambaye anasoma kozi ya muda mfupi ( DMO) ambayo imedhaniwa na ofisi ya Waziri mkuu na mafunzo yao yameaza Juni sita mwaka huu na wanamalizi Disemba 12 mwaka na kozi hiyo ililenga mafunzo ya ufundi stadi wa kozi mbalimbali ikiwamo Umeme.Selemala, Fundi magari .Uwashi., na ujenzi hivyo wanatoa shukrani kama watanzania ofisi ya Waziri mkuu kwa kudhamini mafunzo hayo kwani wengine walikuwa hawana uwezo wa kugharamia mafunzo hayo.
Naye Mwanafunzi Mungine Raines Oscar Amesema kuwa yeye anasoma kozi ya Ukutubi kwa miwili na nusu hivyo wanampongeza kwa kazi kubwa anayoifanya na Mwenyemungu ambariki sana kwani anachokifanya anakwenda kugusa Maisha ya watanzania masikini
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa