Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online,Tanga
Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro itatumia siku ya wapendanao (Valentine Day) kutangaza mapango ya Amboni kupitia Programu ya Diko la Amboni,ambayo itahusisha mashindano ya kupika vyakula vya asili ikiwa ni sehemu ya kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi.
Hayo yamezungumzwa Januari 26,2025, na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhar Kubecha,kwenye mkutano na waandishi wa habari,uliofanyika kwenye mapango hayo na kuhusihusisha vikundi mbalimbali vya ngoma za asili.

Kubecha amewahimiza wakazi wa Wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi na kusherehekea siku hiyo kwenye mapango ya Amboni, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utalii wa ndani.Huku qakitumia uwepo wa siku hiyo kutangaza vitu vingine vya asili ikiwemo vyakula.
“Kutakuwa na mashindano ya wapishi,mavazi wale wenye mavazi ya asili wajitokeze kwakuwa nayo yatahusishwa siku hiyo,kama ambavyo mimi hapa leo nimevaa msuli na kanzu vyote hivi ni kuonesha kwamba jambo hili tunalithamini, “alisisitiza Kubecha.
“Kwakweli siku hiyo ambayo tutashindanishwa mimi nitaomba jiko,ili niingie jikoni na mimi nioneshe uhodari katika kuchangamsha utalii wa mapishi Tanga,”amesema Kubecha.
Pia amesema,jambo hilo litaongeza utalii wa vipando kama baiskeli usafiri ambao zamani ulikuwa ndio pekee kwa jamii ya watu wa Pwani,huku akisisitiza siku hiyo watu wafike kwenye mapango hayo kwa kutumia usafiri wa baiskeli.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, anayeshugjulikia huduma za utalii, Mariam Kobelo, amesema lengo la siku hiyo ni kuiweka jamii pamoja na kukitangaza kivutio cha Amboni wakiamini Tanga ndipo mapenzi yalipozaliwa ,na kwamba wapo sehemu sahihi kutumia siku ya wapendano kutangaza kivutio hicho.

Amesema shughuli hiyo ambayo itafanyika rasmi Februari 14,mwaka huu wanaamini itakwenda kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja pia Mkoa wa Tanga.


More Stories
UVCCM waonywa kuwa ‘machawa’
Wahifadhi Wanawake wa TAWA Watembelea Pori la Akiba Wami-mbiki
Halmashauri Rungwe yapongezwa nafasi ya kwanza matokeo kidato cha nne