Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala Leo imepokea wanachama 388 Kata ya Mzinga katika ziara ya kamati ya Utekelezaji Wilaya ikiongozwa na mwenyekiti wake ndugu Neema kiusa kuwashukuru Wanachama .
Akipokea Wanachama wapya Mwenyekiti wa Umoja wanawake Wilaya ya Ilala Neema Kiusa aliwapongeza Kata ya mzinga kwa kupokea Wanachama wengi kwani wanawake ni Jeshi kubwa .
“Kata ya Mzinga hongereni sana mmefunika mkutano huu leo tumevuna Wanachama wengi Ili ni Jeshi letu naomba Wanawake wezangu mmepandane pia tufanye siasa na uchumi “alisema Neema
Mwenyekiti Neema aliwataka Uwt Mzinga kufuata kanuni na taratibu za chama sambamba na kuimarisha uhai wa Jumuiya hiyo ya Uwt .
Aliwataka Wanawake kuwa wabunifu
katika kubuni Miradi ya Maendeleo Ili waweze kujikwamua kiuchumi .
Alisema dhumuni la ziara hiyo ni kuwashukuru Wanachama kwa kuwapa ushindi wa kishindo pamoja na kuwataka wanawake wa UWT kutangaza mazuri yanayofanywa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Utekelezaji wa miradi ya maendeleo .
Aidha aliwataka Wanawake wa UWT kuweka utaratibu wa kufanya ziara kutembelea makundi maalum .
Katibu wa Umoja wanawake UWT Mzinga Frola Lemu alisema wamepokea wanachama wapya 388 Leo wa matawi mbalimbali ambao wamekabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa Wilaya Neema Kiusa .
Katibu Frola Lemu alisema UWT Mzinga kwa Sasa inajivunia mafanikio makubwa kwa kuwa na mtaji wa kutosha wa Wanachama wa uwt pia Ina mahusiano mazuri ndani ya chama na Serikali .
Diwani wa Mzinga Job Isac alisema anaunga mkono juhudi za UWT mwaka 2024 wajitokeze Kwa wingi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa atawaunga mkono .
Diwani Job Isac alimpongeza MWENYEKITI wa uwt na kamati yake ya Utekezaji na kuwaomba wapange ziara nyingine watembelee miradi ya Maendeleo waangalie Utekelezaji wa Ilani ya ccm.
Kaimu Katibu wa uwt WIlaya ya Ilala Mariamu Bakari aliwataka Uwt kuhakiki mashina yote ya umoja Wanawake UWT na Kufanya Uchaguzi wa mashina .
More Stories
Ilemela nyama choma festival, yazinduliwaÂ
Mchengerwa:Rufaa 5,589 za wagombea zimekubaliwa
Muhimbili yatoa orodha ya Majeruhi ajali ya kuporomoka kwa jengo kariakoo