December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uwoya hapendi kushika simu ya mwanaume

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa filamu mwenye mvuto wa hali ya juu na

mfanyabiashra hapa nchini Irene uwoya amesema hawezi

kushika simu ya mwanaume wake katika maisha yote hata

kama mwanaume amesafiri mwaka mzima.

Akiweka wazi hilo Uwoya amesema, mbali na kutoshika

simu pia hapendi kuambiwa mtu wake yupo sehemu flani

anafanya kitu flani, hata kama atakuwa yupo gesti na

mwanamke mwingine badala yake atajikausha na kujifanya

hajasikia.

Kauli ya Uwoya imekuja, kufuatia nyakati hizi ambapo

simu zinatajwa kuwa chanzo kikuu cha migogoro mingi ya

kimapenzi kiasi cha wengine kufikia hatua ya kutoana

roho.