Na Lubango Mleka, Timesmajiraonline,Kilimanjaro
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepunguza rufaa za wagonjwa nje ya nchi kwa asilimia 97 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya.
Hayo yamesemwa Agosti 11, 2024 Mkoani Kilimanjaro na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na viongozi wa kata 170 katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Aidha Dkt. Mollel alisema Serikali imewekeza teknolojia ya kisasa katika Hospitali zote nchini ikiwa ni kutekeleza uboreshaji wa huduma za afya kwa jamii ili kila mwananchi apate huduma bora za afya.
“Tumepunguza rufaa za nje kwa asilimia 97, wanaokwenda nje kwa ajili ya matibabu ni asilimia tatu huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt Samia, Rais wetu ameleta hospitali nzuri na vifaa tiba vya kutosha ili kuleta huduma bora kwa wananchi,” alisema Dkt Mollel.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam