Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Misungwi
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Emmanuel Masangwa,amesema mazingira ya uwekezaji yaliowekwa na Serikali yatasaidia kukuza uchumi wa wilaya hiyo na taifa kwa ujumla.
Huku uwekezaji uliofanywa na Fulano wa kituo cha mafuta utachochea maendeleo na kukuza uchumi wa Wilaya ya Misungwi.
Masangwa ametoa kauli hiyo Februari 18,2025,Usagara wilayani Misungwi,wakati akizindua kituo cha mafuta cha Fulano Petrol Oil kuwa, Serikali imeweka miundombinu wezeshi kwa wafanyabishara wakubwa na wadogo hasa wazawa, ili kukua kibiashara na kuongeza mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi ikiwemo Wilaya ya Misungwi.

“Uwekezaji huu umetupa heshima,naamini utakuwa na tija kwa wana Usagara na Misungwi kwa ujumla,niwaombe wadau wengine waje kuwekeza na tunawakaribisha,”amesema Masangwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fulano Petrol Oil, Stepheno Fulano,amesema kufunguliwa kwa fursa za biashara kwa wawekezaji wakiwemo wazawa kupitia sera za Serikali,kumemsukuma kuwekeza katika biashara ya nishati ya mafuta.
Fulano amesema ,malengo yake ni kukua kiuchumi na kujitanua zaidi kibiashara,kutoa ajira kwa wananchi,huduma kwa jamii na kupunguza changamoto za kijamii.

Awali Paroko wa Parokia ya Ilemela, Padri Evarist Shigi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha Fulano Petrol Oil amesema,”Mungu alituweka juu ya kazi ya mikono yake na kutuagiza kufanya kazi halali ili kutafuta riziki na kipato,hivyo Fulano umejitoa kuboresha maisha ya jamii ya Misungwi kutokana na biashara ya kuuza nishati ya mafuta,”.
More Stories
Dkt.Mpango aipongeza STAMICO kuwa mfano bora utekelezaji matumizi nishati safi ya kupikia
Wezi wa mapato manispaa Tabora kukiona cha moto
Uwindaji wa kitalii kuingizia Tanzania Bil.2.5