Na Rose Itono,TimesMajira Online. Dar
UMOJA wa Wanaharakati Wazalendo Siasa Tanzania (UWAST) ambao wajumbe wake wanatoka vyama mbalimbali vya siasa nchini, umesema lengo la kuanzishwa kwake ni kutaka kutoa elimu kwa wananchi kudumisha amani.
Akizungumza na waandishi wa habari Kiongozi Mkuu wa Umoja huo, Kunje Ngombale Mwiru amesema licha ya kutoa elimu ya amani kwa wananchi, lakini pia upo kwa ajili ya kuwaonya wanasiasa wanaojaribu kufanya siasa zenye viasharia vya chuki na uchochezi.
“Amani ni neno lenye tafsiri nyingi, lakini amani ikishatoweka hairudi tena hivyo tunatakiwa kuilinda kama mboni ya jicho,” amesema Ngombale.
Ameongeza; “Ni hivi karibuni kiongozi mmoja wa kambi ya upinzani alitoa kauli tata hasa alipovibatiza baadhi ya vyama vya upinzani kuwa ni vyama bandia, jambo ambalo halitofautiani na matusi ya nguoni. Vyama alivyobatiza jina hilo ni vile vinavyokemea kampeni za chuki na viashiria vya uchochezi”.
Amesema UWAST inasisitiza amani kwanza mengine ni maisha baada ya siasa, hivyo kwa kuilinda amani iliyopo inatakiwa watu bila kujali ukubwa wa chama, urefu au upana wa chama kujua thamani ya Watanzania.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza