Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amesema kuwa kilo za mabondo zilizosafirishwa kwenda soko la nje ya Nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwanza zimeongezeka kutoka kilo 431,721 mwaka 2020 hadi kilo 495,448 mwaka 2024 sawa na ongezeko la kilo 63,727.
Mtanda amesema hayo jijini hapa leo,Julai 16,2025 wakati akizungumza na waandashi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ambapo amesema kuwa hayo ni kutokana na kuongezeka kwa Ufugaji wa samaki kwa kutumia njia ya kisasa kutoka vizimba (fish cauges) 1,664 mwaka 2020 hadi 2,715 mwaka 2025 sawa na ongezeko la vizimba 1,051.

Vilevile amesema jumla ya tani 43,657.6 za minofu ya Samaki zimechakatwa na tani 81,812 zimesafirishwa kwenda soko la nje ya Nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kipindi cha mwaka 2024.
“Idadi ya mabwawa ya ufugaji wa Samaki imeongezeka kutoka 286 mwaka 2020 hadi mabwawa 531 mwaka 2025 sawa na ongezeko la mabwawa 245,”amesema
Aidha amesema kuwa maongezeko hayo yamefanya kiasi cha mapato yaliyotokana na shughuli za uvuvi kumeongezeka kutoka Shilingi 4,416,172,821.59 mwaka 2020 hadi Shilingi 8,233,724,351.33 mwaka 2025 sawa na ongezeko la Shilingi 3,817,551,529.74.
Pamoja na hayo Mtanda amesema ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri za Mkoa huo yameongezeka kutoka shilingi Bilioni 44.2 mwaka 2020/2021 hadi shilingi Bilioni 70.7 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 60.
Amesema katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita mkoa huo umepokea jumla ya shilingi Trilioni 5.6 kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya na Elimu.

“Makusanyo yameongezeka kutoka jumla ya Shilingi Bilioni 44.2 mwaka 2020/21 hadi Shilingi Bilioni 70.7 mwaka 2024/25 kufikia mwezi Mei, 2025 sawa na ongezeko la 60%,kwa kipindi cha miaka mitano zimekusanywa jumla ya Shilingi Bilioni 216.2.
“Jumla ya Shilingi Trilioni 5.6 zimepokelewa Mkoani kipindi cha mwezi Novemba, 2020 hadi Aprili, 2025 kwa ajili ya maendeleo ya sekta mbalimbali ambapo jumla ya shilingi bil.63.2 zimetolewa sekta ya Afya na kywasaidia wananchi kuoata huduma kirahi,”amesema.
Mtanda amesema kiasi cha shilingi bil. 196.8 kimepelekwa sekta ya Elimu na kuboresha miundombinu ambayo imesaidia kupunguzia wanafunzi kutembea umbali wa mwendo mrefu kufuata shule,msongamano wa wanafunzi madarasani na kuwezesha mazingira bora zaidi kwa walimu na wanafunzi.
“Maboresho yafuatayo ni pamoja na mpango wa Elimu Bila Malipo kwa shule za msingi katika Mkoa umegharimu jumla ya Shilingi 32,812,096,940.45 kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2024/2025,idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka shule 873 mwaka 2020 hadi shule 930 mwaka 2025, sawa na ongezeko la shule 57,”amesema.
Aidha amesema kiasi cha shilingi bili 156.3 kimetekeleza miundombinu ya barabara na baadhi ya miradi iliyotekelezwa na TANROADS ya gharama ya Shilingi bil. 36.9,ambapo fedha hizo zimesaidia kukarabati na kujenga madaraja 13 likiwemo Daraja la Simiyu,Sukuma,Mabatini na Mkuyuni.
“Daraja la Simiyu linajengwa kwa gharama ya Shilingi bil.4.8,Daraja la Sukuma: linajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 9.4,Daraja la Mabatini: linajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6 na Daraja la Mkuyuni: linajengwa kwa gharama ya Shilingi bil. 5.2,”amesema.

More Stories
Mfanyabiashara,vibarua mbaroni wakituhumiwa kuchimba mahandakiÂ
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8