Na Penina Malundo,timesmajira,Online
MKOA wa Mtwara ni miongoni mwa mikoa inayovunwa madini Chumvi ikifuatiwa na mikoa ya Kigoma,Simiyu,Tanga,Dar es Salaam pamoja na Lindi.
Matumizi ya chumvi nchini yanakadiriwa kufikia tani 500,000 kwa mwaka huku uzalishaji wake nchini kuonekana kupanda kutokana na wakulima wa mikoa hiyo kuongeza kasi ya ulimaji.
Uvunaji wa chumvi ni fursa pekee kwa wananchi wanaofanya shughuli hiyo kwani utumika kama kiungo cha chakula kwa kuongezewa madini joto “IODINE”.
Pia Chumvi kama kutumika kama kiungo cha chakula cha binadamu na mifugo,hutumika pia katika viwanda vya minofu ya Samaki,usindikaji wa nyama,usafishaji wa maji,utengenezaji wa karatasi,uchimbaji wa visima vya gesi na mafuta.
Asilimia kubwa ya watu wanaofanya uzalishaji wa chumvi nchini ni watu wenye kipato cha chini hivyo ukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa vibali,miundombinu ya uvunwaji wa chumvi pamoja na vitendea kazi.
Viongozi wa maeneo mbalimbali ikiwemo katika serikali za vijiji na halmashauri nao wamekuwa watu wa kuwarudisha nyuma wazalishaji hao kwa kuwawekea vikwazo mbalimbali.
Abdallah Lipapike ni mmoja wa wanakikundi wa Kikundi kiitwacho Hiari kinachojishughulisha na uvunaji wa Chumvi katika kijiji mboji kitongoji cha mkolesala Mkoani Mtwara,anasema kikundi chao kilianzishwa mwaka 2017 huku mradi wa uvunwaji wa chumvi walianza rasmi mwaka 2020.
Anasema baada ya kuona kuna fursa kubwa katika uvunaji wa chumvi kikundi chao cha watu tisa,wanawake wakiwa wanne na wanaume wakiwa watano waliamua kujikita katika mradi huo wa uvunaji wa chumvi kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Anasema wameanzisha kikundi hicho kwa dhamira kubwa ya kujikwamua kiuchumi kutokana na hali zao duni na kufikia katika kipato cha kati ili kuweza kusaidia familia zao zinazowategemea.
“Dhamira yetu kubwa ya kikundi hiki ni kujikwamua kutoka katika hali ngumu ya uchumi na matarajio makubwa ni kutoka pale tulipoanza na kufikia katika Maisha ya kati,”anasema.
Anasema licha ya kuwa na ndoto hizo za kuwa na kipato cha kati kwa kutegemea mradi wao huo mkubwa wa lakini wamekuwa wakikabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo ya upatikanaji wa leseni ya madini katika uchimbaji wa madini hayo ya chumvi.
“Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni upatikanaji wa leseni za madini katika uvunaji wetu wa chumvi,hivi vitu vinatubana na kutupa changamoto katika kufanya shughuli zetu kwani tunakuwa hatutambuliki rasmi,”anasema na kuongeza
“Tunaomba Serikali itusidie na kuingilia kati kutuangalia kwa jicho la karibu sisi wajasiriamali wa vijijini tunakubwa na changamoto sana ya vibali hivyo,”anasema
Anasema madini hayo ya chumvi yanafaida kuwa sana kwani katika kijaruba kimoja wanauwezo wa kuvuna mara tatu hadi nne.
Lipapike anasema tangu mwaka jana walipoanza mradi huo wa uvunaji wa Chumvi walikuwa wanatamani kusajili kikundi chao ila changamoto mbalimbali ikiwemo ucheleweshewaji wa vitambulisho vya ujasiriamali nayo ilikuwa mojachangamoto mbalimbali ikiwemo ucheleweshewaji wa vitambulisho vya ujasiriamali nayo ilikuwa moja ya changamoto ambapo hadi sasa hawajapatiwa licha ya kulipia vitambulisho hivyo.
Anasema tayari wamelipa fedha kwa Mtendaji wao wa Kijiji, lakini vitambulisho hivyo vimechelewa kuwafikia hadi sasa na kukwamisha mipango yao mingi ikiwemo ya upatikanaji wa vibali vingine.
MRADI WA CHUMVI ULIPOANZA
Anasema kutokana na kuona elimu yao kuwa ndogo kwao na kuona shughuli za kilimo pekee haiwezi kuwasaidia kupata fedha nyingi waliamua kujiunga kama kikundi na kuanza harakati za uvunaji wa chumvi.
Anasema walipokuwa katika maandalizi hayo,walibahatika kutembelewa na Shirika linalopambana na kupiga vita umasikini nchini( MSOWAPO) ambalo liliwasikiliza changamoto zao na kuamua kuanza kuwasaidia katika mradi wao wa uvunaji wa Chumvi na ufugaji wa Samaki.“Shirika la MSOAPO limetusaidia kwa kiasi kikubwa kufikia hapa tulipo katika mafanikio yetu licha ya kukabiliana na changamoto ya vibali,”anasema.
Anasema Shirika la MSOWAPO limewasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kuwapatia vitendea kazi mbalimbali ili kuweza kuwarahisishia katika kazi zao.
Anaeleza miongoni mwa vitu ambavyo shirika liliwaletea ni pamoja na mashine ya kuvuta maji,paipu ya kuvuta maji na kuyaweka katika vijaruba,viatu vya kuingilia katika maji ,miwani,Chepe za kuchimbia
mchanga.
“Baada ya kupata vifaa hivi,tumeona ndoto zetu zimeanza kutimia sasa tayari tumeajiri watu 30 katika kufanya shughuli hii na tutaendelea kuajili wenzetu,”anasisitiza na kuongeza
“Unajua mwaka jana tulipoanza hatukupata kitu kutokana na miundombinu yetu kuwa duni,I;la mwaka huu tayari tunachumvi nyingi tuliyoivuna ipo katika gala na hapa bado nyingine ipo katika vijaruba tunahakika tutapata zaidi ya tani 5000 kwa mwaka huu,”anasema.
Anasema wakiuza chumvi hiyo watasomesha watoto wao,watapata fedha za kujikimu kimaisaha na kupata maendeleo,”anasema
Anasema kabda ya MSOWAPO kuwafikia katika kuwasaidia katika mradi wao wa Chumvi walifanikiwa kujenga vijaruba vinne ambapo na wao wamewaongezea vinne na kuwa nane.
“Kila kijaruba kimoja cha chumvi tunatarajia kutoa chumvi viroba vya kilo 50 takribani 300 na kuhusu soko tutaangalia kulingana na bei kwani tayari tunagala la kuhifadhia Chumvi hiyo,” anasema.
Naye Mwenyekiti wa Kikundi hicho,Mussa Mduma anasema katika miradi hiyo hawapo pekee yao bali pia wapo wanawake ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kufanya shughuli hizo
“Tumeamua kuingiza wanawake katika kikundi chetu katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita ya ushirikishwaji wa wanawake katika nyanja mbalimbali na hata Rais Samia Suluhu Hassan mara nyingi anaagzia uwepo wa usawa katika shughuli mbalimbali,”anasema.
Naye Mratibu wa Shirika la MSOWAPO,Mustapha Kuyungwa anasema shirika lao nililiona linaweza kuwasaidia kwa sababu ni kundi ambalo lilikuwa na uhitaji maalum katika kusaidiwa kwenye maeneo mbalimbali ili kuweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.
Anasema Shirika liliweza kuwatembelea na kugundua kuwa wanachangamoto mbalimbali hivyo walikaa nao na kuchukua mahitaji yao wanayohitaji katika kuwaboreshea miundombinu ya kilimo cha Chumvi .
“MSOWAPO tuliweza kuwasaidia kipimo cha kupima Ubora wa Chumvi wanaovuna kwa kuangalia madini wanayoyatumia,”anasema na kuongeza.
“Pia walikuwa wanahitaji pumpu ya kujazia maji katika vijaruba,Viatu vya kuingilia kwenye maji,machete,miwani pamoja kuwatengenezea gala la kuhifadhi Chumvi pindi mvua inaonyesha,”anasema.
Anasema mwaka jana walilima na kubahatika kupata Chumvi lakinj
mwishoni walipata hasara baada ya mvua kunyeshea na kuharibika.
Anasema Shirika lao baada ya kuona hali hiyo mwaka huu ikaona iwasaidie kutunza Chumvi na kuweza kukaa kwa mtu mrefu na kuweza kutafuta masoko kwa uhakika zaidi.
“Changamoto ambayo wanakumbana nayo wakulima hawa wa Chumvi ni uwepo wa bei ndogo katika kipindi cha kuvunay kwahiyo anauza bei ambayo haina tija,”anasema na kuongeza
“Kutokana na kukiwezesha kikundi chao cha hiari na kupata gala kwa sasa watakuwa wanahifadhi Chumvi kwa muda mrefu na kutafuta soko la uhakika zaidi hata Chumvi ikikaa katika gala hiyo miaka miwili lakini bado wanauza kwa bei Nzuri,”anasema.
Aidha anasema Shirika lao linashauri wananchi kuungana na kukaa kwenye vikundi katika kupambana na umasikini katika jamii yao ili kusaidia kuwavutia wawekezaji au wadau ya maendeleo kuwasaidia kwa urahisi.
More Stories
Boost ilivyoboresha miundombinu ya elimu Ilemela
Samia apongeza walimu 5,000 kupatiwa mitungi ya gesi, majiko kutoka Oryx
Uwekezaji kwenye kilimo utatimiza ndoto ya Samia ya nchi kuwa ghala la chakula Afrika