Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online. Songea
WAJUMBE wa Jumuita ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Songea Mjini wamemchagua Kelvin Chale kuwa Mwenyekiti baada ya kuwabwaga washindani wenzake kwa kura 185.
Uchaguzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Open University Manispaa ya Songea kwa lengo la kuziba pengo la nafasi ya Mwenyekiti baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Issa Chiwaneke kushinda Udiwani Kata ya Ndilima Litembo.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mwanahamisi Manyopo amesema Chale amekuwa mshindi baada ya kupata kura 185, Kalela Khalifa kura 130 akifuatiwa na Renatus Chale kura 32 na Rustika Komba aliyepata kura moja.
Amesema wajumbe waliopiga kura ni 354 huku kura zilizoharibika ni sita na kura halali 348.
Kwa upande wake Mwenyekiti aliyechaguliwa, Chale amesema atahakikisha anawapigania vijana kupata mkopo asilimia nne kutoka halmashauri, ili ziwasaidie kuanzisha biashara ndogo ndogo.
Amesema atatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa kushirikiana na viongozi wenzake, ili mikopo watakayopata iwe na manufaa kuinua uchumi wa vijana ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha kwani jumuiya hiyo kwa saaa imegawanyika, yeye atawaunganisha na kuwaletea maendeleo.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari