TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavYo:-
- Amemteua Bw. Andrew Wilson Massawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). Bw. Massawe anajaza nafasi ya Dkt. Tausi Mbaga Kida aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uwekezaji.
Uteuzi huo umeanza tarehe 02 Aprili, 2023; na
- Amemteua Prof. Ulingeta Obadia Lebson Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kipindi cha miaka mitatu (03). Prof. Mbamba anachukua nafasi ya Prof. Blasius Bavo Nyichomba ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi huo umeanza tarehe 29 Machi, 2023.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

More Stories
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Baraza la Taifa la Ujenzi waingia makubaliano ya mashirikiano sekta ya ujenzi
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani
Taarifa za maendeleo ziwafikie wananchi kwa usahihi