Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
Aidha Utafiti huo umeonyesha kuwa mwaka 2020 Tanzania ilitumia dola milioni 700 kugharamia katika kukinga na kutibu magonjwa hayo.
Akizungumza katika mkutano wa kutoa ripoti ya matokeo ya utafiti katuika sekta ya afya uliofanywa na watafiti mbalimbali hapa nchini, Profesa Goodluck Makundi alisema, magonjwa yasiyo ya kuambukiza hapa nchini bado ni changamoto.
“Kuna ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa nchini Tanzania na kufikia vifo,ongezeko hili ni mara mbili ya hali ilivyokuwepo mwaka 2015,hali hii inasababisha nguvu kuelekezwa zaidi katika kutibu kuliko kukinga ,na ni ghali kutibu kuliko kukinga.”
Profesa Makundi alisema tatizo hilo haliwakumbi watu wazima na wazee tu bali hata vijana na watoto wanakumbwa huku akisema linachangiwa sana na mabadiliko ya mtindo wa maisha na lishe .
Aidha alisema,hilo ni tatizo mtambuka linahusisha sekta mbalimbali.
“Ni changamoto kubwa hapa nchini kwa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza ,magopnjwa haya ni pamoja na moyo,shinikizo la damu,saratani mbalimbali pamoja na magonjwa ya mfumo wa hewa.”alisema na kuongeza kuwa
Profesa Goodluck alitaja baadhi ya vitu vinavyosababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kuwa ni pamoja na matumizi ya tumbaku,kutofanya mazoezi,ulaji vyakula usiozingatia lishe bora na matumizi ya pombe kupita kiasi.
Alisema,Shirika la Afya Duniani linasema,mambo hayo yanachangia kwa asilimia 80 ya tatizo hilo duniani.
Akizungumzia kuhusu matokeo ya utafiti uliofanywa na watafiti katika sekta ya afya alisema,matatizo ya magonjwa hayo yasiyo ya kuambukizwa na majeruhi inachangia kwa asilimia 41 ya vifo na walemavu.
Vile vile alisema,matokeo ya utafiti wao umeonyesha,pamoja na mambo mengine kuna upungufu wa fedha za kugharamia magonjwa hayo ambapo asilimia 7.8 ya matumizi ya sekta hiyo ndio hutumika ikilinganisha na tatizo la asilimia 41 .
Akitoa mapendekezo katika sekta ya afya alisema,inahitaji uratibu wa hali ya juu kwa kutumia ofisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Rais Tamisemi,lakini pia sheria na kanuni zilizopo dhidi ya mapambano ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ziimarishwe .
“Mfano bidhaa za mazao ya tumbaku ziongezwe kodi pamoja na kupiga marufuku matangazo yake.”
Vile vile alisema pendekezo linguine ni kuanza kuzungumzia elimu ya magonjwa haya katika ngazi tofauti tofauti,pia yaingizwe kwenye mpango wa elimu ya afya mashuleni.
Profesa Makundi pia alisema pendekezo linguine ni ,vyombo vya habari vikiwemo vya mitandao ya kijamii ,vilete mabadiliko kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na magonjwa hayo.
“Social media(mitandao ya kijamii) inaweza kutumika ‘positively’…,maana media ni eneo ambalo tukishirikiana vizuri linaweza kuleta matokeo chanya .”alisisitiza
Pia alisema watafiti katika eneo hilo la afya wamependekeza kuwepo na uwekezaji zaidi huku akisema,kuna haja ya kutafiti zaidi na kuwekeza kwenye utafiti ili kutatua matatizo hayo lakini pia kuna haja ya kutumia maafisa maendeleo ya jamii kuelimisha watu katika ngazi tofauti tofauti.
Katika hatua nyingine alisema viongozi wa dini pia wanao wajibu wa kuelezea angalau kwa dakika chache wawapo katika ibada zao huku akisema,hii itasaidia waumini kupata uelewa juu ya magonjwa haya katika maeneo tofauti tifauti a kuwapa uelewa wa kutosha.
“Kwa hiyo tunaona kuna haja ya kutumia majukwaa tofauti tofauti katika kupambana na magonjwa haya,lakini pia kila mtu ahusike katika kuchukua hatua ikiwemo kufanya mazoezi,pia taasisi mbalimbali zikiwemo shule shule nazo zina jukumu la kuhamasisha mazoezi..,pia vyakula vyakula nyumbani vizingatie suala la lishe .”alisisitiza Profgesa Makundi
Awali akifungua hafla hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COASTECH) mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa COASTECH Dkt.Wilbert Manyilizu alisema, lengo la warsha hiyo ni kuwashirikisha Wadau wakuu wa matokeo ya tafiti za kisayansi na Teknolojia ili waweze kuwasilisha na kutoa matokeo ya tafiti zao.
Alisema,Coastech iliwaita watafiti katika Sekta nne za awali ambazo ni sekta ya Afya,Kilimo,maliasili na mifugo ili wawasilishe tafiti zao ambazo hufanyiwa kazi na Tume hiyo ambayo ndio yenye dhamana ya kuishauri Serikali katika masuala ya sayansi na teknolojia.
Aidha alisema,lengo la kuanzishwa kwa Tume hiyo ni kuishauri Serikali katika masuala ya sayanasi na Teknolojia na ubunifu huku akisema,jukumu kubwa la COASTECH ni kuratibu na kuhamasisha Mambo ya utafiti na ubunifu ambapo katika jukumu hilo pia kuna majukumu mengine.
Ameyataja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kusimamaia Menejimenti ya maarifa yanayopatikana katika ubunifu na utafiti na baadae kusambaza kwa Wadau huku akisema, michakato yote ya kuwatambua na kuwawezeaha wabunifu ni jukumu lao.
Aidha alisema,jukumu linguine la Tume hiyo ni kuhabarisha Wanachi na Wadau mbalimbali kwa kukusanya na kusambaza taarifa za sayansi na ubunifu wa wananchi pamoja na kusambaza vijarida.
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25