January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ushetu kujengwa kituo kidogo cha kupozea umeme

Na Joyce Kasiki,Dodoma

SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO) lina mpango wa muda mfupi wa Kujenga kituo kidogo cha kupozea umeme katika eneo la Nyamirangano Halmashauri ya Ushetu .

Hayo ymesemwa.leo Nov 2,2023 na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga bungeni jijini Dodoma wakati Akijibu swali la Mbunge wa Ushetu Emmañuel Chereheni ambaye katika swali lake alitaka kujua mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme katika halmashauri za Ushetu ,Msalala na Kahama .

Kapinga amesema kupitia kituo hicho TANESCO itaongeza njia nyingine kutokea halmashauri za Ushetu,Msalala na Kahama ambazo zitasaidia kuboresha upatikanaji wa umeme huku akisema mradi huo wenye thamani ya shilingi bili 1.2 inatarajiwa kukamilika 2024.

Akiuliza swali la.nyongeza Cherehani amesema Hali ya umeme katika wilaya Kahama imekuwa ni shida na hivyo kupeleka wafanyabiashara kushinda wamekaa siku nzima bila kufanya kazi kutokana na kukatikankwa.umeme kutwa nzima.

Cherehani pia ametaja kujua kama Naibu Waziri huyo yupo tayari kwenda kujionea Hali halisi lakini pia ametakq kujua mkakati wa Serikali wa kuipa wilaya ya Kahama kuwa.mkoa wa KITANESCO kutokana na eneo hilo kukua kwa kasi .

Akijibu maswali hayo Kapinga amesema yupo tayari kwenda Kahama kujionea Hali halisi ya kukatika kwa umeme lakini amesema Serikali itaendelea kuona kama Kahama inafaa kuwa mkoa wa KITANESCO.

Aidha Kapinga ameilekeza TANESCO na kituo kidogo Cha pamoja Cha Grid ,wahakikishe maeneo yote yanapata umeme kulingana na maboresho yanayofanyika