January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Urambo,Kaliua kupitia upya mipaka ya kiutawala

Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Kaliua

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora Grace Quintine amesema wamefanya kikao cha ujirani mwema na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ili kupitia upya mipaka ya kiutawala kati ya Wilaya ya Urambo na Kaliua ili kurahisisha huduma kwa wananchi.

Quintine amesema kikao hicho kimewakutanisha viongozi wa Wilaya zote mbili ambazo ni Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na wataalam mbalimbali wakiwemo wa ardhi kwa lengo la kuweka usawa wa jambo hilo ili jamii iweze kuondokana na hali ya sintofahamu.

Amesema wakiwemo katika kikao hiko wamefanikiwa kujadili mambo muhimu kama ustawi wa jamii kwani Wilaya ya Urambo na Kaliua ni majirani , hivyo basi wananchi wa Wilaya hizo mbili ushirikiana katika shughuli mbalimbali kama za kiuchumi ikiwepo biashara.

“Kupitia kikao hiki tumekubaliana kwamba Wataalamu wetu wa Idara ya Ardhi kushirikiana kupitia upya maeneo yetu ya Kiutawala hasa tunapoeleke kwenye Chaguzi Mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amezishukuru Kamati za Ulinzi na Usalama zote mbili chini ya Wakuu wa Wilaya akiwepo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Elibariki Bajuta Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kaliua kwa kusimamia vyema kikao hiko huku wakiwemo Viongozi wengine mbalimbali kwa Ushirikiano mwema kuwahudumia Watanzania kwa ufanisi mkubwa.

” Binafsi nizishukuru Kamati zote mbili za Ulinzi na Usalama za Wilaya zetu chini Wakuu wa Wilaya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Elibariki Bajuta Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kaliua kwa kusimamia vyema kikao chetu kimeenda vizuri na Viongozi wenzangu kwa Ushirikiano mwema kuwahudumia Watanzania kikamilifu ” amefafanua Quintine.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ya kipekee ya kuendelea kuwapatia miiradi Mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na Kaliua.