Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalum . Tecla Ungele, amepongeza kwa nguvu mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sekta ya afya nchini chini Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Ungele ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Afya ambapo amesema,
mafanikio ya kupunguza vifo vya uzazi kutoka wanawake 556 kwa kila vizazi hai 100,000 hadi kufikia vifo 104 hadi kufikia Februari 2025 ni hatua kubwa isiyo ya kawaida.
”Na hii ndiyo sababu Rais Samia Suluhu Hassan alipata ‘Global Goalkeeper Award’ kutoka taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation.”amesema na kuongeza kuwa
”Haya ni mageuzi makubwa ambayo hatujawahi kuyashuhudia kwa miaka mingi,kupungua kwa vifo vya wajawazito kwa kiwango hiki si jambo dogo, tunampongeza sana Rais wetu kwa uongozi wake wa kipekee,” amesema . Ungele.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuendelea kuboresha vifaa tiba katika vyumba vya uzazi na huduma za watoto wachanga, hususan kwenye maeneo ya vijijini na pembezoni.
Amesema kuwa vifaa hivyo ni muhimu katika kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma bora, salama na za haraka.
Ungele pia alipongeza kazi kubwa inayofanywa na wauguzi nchini, akisisitiza kuwa elimu ya uuguzi iendelee kutolewa kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa ili kuongeza ujuzi na uwezo wa kutoa huduma bora.
”Kada ya uuguzi ni uti wa mgongo wa huduma za afya.,tunapaswa kuwatambua, kuwathamini na kuwawezesha kielimu na hata kimaisha – maana maeneo mengi hawana hata nyumba nzuri za kuishi,” allmeeleza.
Changamoto za Mkoa wa Lindi
Akizungumzia Mkoa wa Lindi,Ungele aliishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya, ujenzi wa zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na mkoa pamoja na kuwekwa kwa vifaa vya kisasa kama ICU na huduma za dharura.
“Huduma za ICU ni mkombozi wa maisha kwa wagonjwa mahututi. Tunashukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuziweka Lindi. Zinaokoa maisha,” amesema.
Hata hivyo, ameeleza changamoto kadhaa zinazoukumba mkoa huo kuwa ni pamoja na Hospitali ya Mkoa wa Lindi – Sokoine kuwa na majengo chakavu, na kuomba jengo jipya la rufaa linalojengwa eneo la Mitwero likamilishwe haraka ili huduma zitolewe katika mazingira bora zaidi.
“Nilitembelea jengo jipya la hospitali, baadhi ya maeneo bado hayajakamilika. Tunaomba likamilike haraka kwa sababu hospitali ya sasa ni chakavu sana,” amesema.
Madaktari Bingwa na Rasilimali Watu
. Ungele alisifu kampeni ya Dkt. Samia ya kupeleka madaktari bingwa katika wilaya zote, akisema imewasaidia wananchi wengi waliokuwa hawawezi kufikia huduma hizo kwa sababu ya umbali au gharama.
Aliongeza kuwa kampeni hiyo imewawezesha pia wataalamu walioko wilayani kupata ujuzi na maarifa kutoka kwa madaktari bingwa waliotembelea maeneo yao.
Pamoja na mafanikio hayo, alieleza upungufu mkubwa wa rasilimali watu katika mkoa wa Lindi. Alitaja kuwa Hospitali ya Mkoa wa Lindi haina madaktari wa usingizi, mionzi, magonjwa ya ndani, na magonjwa ya masikio, pua na koo.
Aliiomba Wizara ya Afya kuikumbuka hospitali hiyo katika mgao wa madaktari bingwa kwenye mipango ya kuimarisha huduma za afya nchini
”Tuna changamoto kubwa ya rasilimali watu,tunaomba hospitali yetu ya mkoa isahaulike, tupewe madaktari bingwa kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi wetu,
More Stories
Kiongozi wa Mwenge apongeza wananchi kupelekewa huduma ya maji Handeni
TFS yawakaribisha wawekezaji katika vivutio vya utalii wa misitu
Waziri Bashungwa:Tumieni teknolojia za kisasa kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka