January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UN yakaribisha uamuzi wa bunge dogo Somalia

NEW YORK, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Antonio Guterres amekaribisha uamuzi wa bunge dogo la baraza la shirikisho nchini Somalia la kubatilisha sheria maalum na kurejea kwenye mkataba wa uchaguzi wa Septemba 17 ambao utaruhusu kufanyika kwa uchaguzi wa rais na wabunge usio wa moja kwa moja.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu António Guterres amesisitiza wito wake kwa wadau wote wa Somalia kuanza mazungumzo mara moja na kufikia muafaka juu ya kufanyika kwa uchaguzi ulio jumuishi bila kucheleweshwa zaidi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, “Katibu Mkuu anasisitiza umuhimu wa makubaliano yenye wigo mapana zaidi kwa ajili ya utulivu wa nchi,”ameeleza.

Sheria maalum ya uchaguzi wa shirikisho ilipitishwa na baraza la bunge dogo Aprili, ikiruhusu kuongezewa muda kwa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kwa kipindi cha miaka miwili zaidi baada ya muda wake kumalizika rasmi mwezi Februari.