Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Rungwe
UMOJA WANAWAKE wa Chuo cha Magereza Kiwira Wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametoa msaada wa vyakula kwa wazee wasiojiweza katika Kitongoji cha Makandana Kata ya Lupepo katika kusherekea siku ya wanawake duniani.
Msaada huo umekabidhiwa Machi 8,2025 na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira ambaye pia ni Mrakibu Mwandamizi wa Chuo hicho ,Ester Muyombe na kusema kuwa kuanzia walmeona ni kufika Kitongoji cha jirani na Chuo ikiwa ni siku ya kusherekea maadhimisho hayo.
“Tumefika katika Kijiji hichi ambacho kipo jirani na Chuo chetu tumekabidhi msaada wa mchele,nguo, sukari, chumvi na mahitaji mengine muhimu kwa wazee wetu hawa ambao naamini bado kwa siku hii ya leo wamepata faraja kubwa”amesema..
Akielezea zaidi Kaimu Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira amesema kuwa vyuo vyao vya Jeshi la magereza vipo nje ya miji hivyo wahitaji wengi wanaojulikana wapo Mijini katika sehemu wanazokusanywa lakini kama mtandao wetu wakajipanga na kuwafikia wazee ambao wapo Vijijini ambao hawaonekani kirahisi.
Lucy Elia Mrakibu Mwandamizi wa Magereza na Mwenyekiti mtandao wanawake Chuo cha Magereza Kiwira amesema kuwa kitendo cha kuwatembelea wahitaji ni jambo la ibada kutokana na kundi hilo kuishi maisha duni.
“Sisi kama wanawake katika kusherekea sikukuu ya wanawake tumeona ni jambo la msingi tuwaone wazee wetu hawa ambao jirani na Chuo chetu hichi ili tuweze kuwapa faraja kubwa maana wazee ni tunu kubwa hivyo lazima tuwape thamani kubwa”amesema .
Akipokea msaada huo kwa Niaba ya wazee Mwenyekiti wa kitongoji cha Makandana Kata ya Lupepo,Maiko Mbughi amesema kuwa toka kuzaliwa kwake haijawahi kuona wanawake wakiona wazee na kuwapa mahitaji muhimu lakini wao wamethubutu kufanya tendo hilo ambalo ni ibada kwao.
Amesema kuwa mara nyingi kundi la wazee limekuwa katika maisha duni hivyo kilichofanywa na wanawake wa Chuo cha Kiwira kina baraka kubwa kwao na kinapaswa kuigwa na jamii na wadau wengine katika kuhakikisha kuwa kundi la wazee linapewa kipaumbele.


More Stories
Mgao wa tenda wa 30% kwa makundi Maalum ,wamkosha Rais Samia
SBL yatambuliwa Tuzo za Rising Woman
Jeshi la Polisi lamtia mkononi mtuhumiwa wa utekaji