Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameungana na Umoja wa Taasisi za Kiislamu Tanga (SHITTA) kushiriki kwa pamoja kutoa chakula kwa wagonjwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adhaa.
Hata hivyo Mbunge huyo alimpongeza taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na wagonjwa katika hospitali hiyo,kwenye kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dkt.Batilda Burian ameipongeza SHITTA kwa kuungana na wagonjwa hao ambao wengine hawana ndugu wala jamaa kupata sadaka hiyo na kupata faraja.
Pia ameahidi kuipa ushirikiano taasisi hiyo ili iweze kufikia malengo inayokusudia.
Mwenyekiti wa SHITTA Omari Guledi amempongeza Waziri Ummy na Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa namna ambavyo wamewaunga mkono kwenye zoezi hilo muhimu la jamii.
Katibu wa Shirikisho hilo,Ahmed Mustapha ,amesema madhumuni ya kutengeneza umoja huo ni kutaka kufanya taasisi zao ziweze kujitegemea na kufundisha dini hiyo ipasavyo.
Amesema ndani ya taasisi hiyo kuna umoja wa vijana,wanawake na wazee na ikifika mahali pa kutoa huduma hatubagui kuwa tunauemhudumia ni mtu wa imani ipi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa