December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UMAU, Diwani Mtoka wagawa chakula kwa yatima

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Umoja wa marafiki wa Ukonga UMAU kwa kushirikiana na Diwani wa Viti Maalum wa Wilaya ya Ilala Semeni Mtoka, wamegawa chakula kwa watoto Yatima wa kata ya Msongola wilayani Ilala katika madhimisho ya UMAU day.

Msaada huo uligaiwa na kikundi cha marafiki wa Ukonga wakiongozwa na Diwani Semeni Mtoka, kwa kushirikiana na Diwani Mwenyeji AZIZI MWALILE, katika kituo cha yatima Msongola.

Akizungumza wakati wa kugawa chakula kwa watoto yatima Diwani Semeni Mtoka, alisema watoto wa makundi maalum ni muhimu kuwa nao karibu wao ni sawa na Jamii nyingine hivyo wasitengwe.

“Kikundi chetu cha kufa na kuzikana cha marafiki wa ukonga ni cha kijamii kwa kushirikiana na Wanachama wezangu wa kufa na kuzikana tumeadhimisha siku maalum ya UMAU day hivyo tumegawa chakula na watoto yatima wa Msongola na wao wafurahi kama jamii nyingine ambapo tumewapa chakula na kuwafariji ” alisema Diwani Semeni.

Diwani Semeni Mtoka, alisema baadhi ya vyakula walivyotoa msaada katika kituo hicho, Maharage,Mchele,Unga,Mchele, Sabuni na mafuta ya kupikia.

Aliwataka wadau wengine kujenga tabia ya kuwa karibu na vikundi vya watoto yatima kwa ajili ya kuwapa msaada na kuwafariji wajione na wao wanapendwa