Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Madereva 11, mkoani Mwanza wamefungiwa leseni kwa tuhuma za kukutwa wakiendesha vyombo vya moto (magari), wakiwa wamelewa ambapo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani na hatari kwa watumiaji wa barabara.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya oparesheni ilioanza Julai 14,2025,iliofannywa na Jeshi la Polisi ya kuwakamata madereva wanaovunja sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani kwa kufanya matendo hatarishi yanayoweza kusababisha ajali.
Akizungumza na waandishi wa habari,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, amesema katika siku za hivi karibuni,jeshi hilo limebaini kuongezeka kwa ajali za barabarani nyakati za usiku na hata mchana zinazosababishwa na baadhi ya madereva wanaoendekeza tabia ya kunywa pombe na kisha kuendesha vyombo vya moto
na kusababisha ajali.
Ambapo ameeleza kuwa,ajali za barabarani zinaleta madhara ya kupoteza maisha, majeruhi, na wakati mwingine uharibifu wa vyombo na miundombinu ya barabara.
“Vifo au majeraha,vinasababisha kupungua kwa nguvu kazi, uharibifu wa magari unasababisha gharama katika utengenezaji wa magari na kupelekea umasikini kwa wahanga na kuharibika kwa
miundo mbinu ya barabara unasababisha serikali kuingia gharama nyingine katika
kutengeneza miundombinu hiyo.
Mutafungwa amesema,oparesheni hiyo inaendelea katika barabara zote za Mkoa wa Mwanza,ambapo dereva kuendesha gari akiwa amelewa ni kitendo hatarishi kinachoweza kusababisha ajali hivyo wavunjaji hao wa sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani wamekamatwa na
wanaendelea kuhojiwa ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.
Amewataja,watuhumiwa waliokamatwa katika opareshheni hiyo waliokuwa wakiendesha gari huku wamelewa pamoja na hatua za kisheria walizochukuliwa ikiwa ni pamoja na kufungiwa leseni ya kuendesha gari na vyombo vingine vya moto vinavyotembea barabarani kwa kipindi cha
miezi mitatu kuanzia Julai 21,2025.Adhabu hiyo ni kwa wote 11, akiwemo Gesase Maiko(51), mfanyabiashara na mkazi wa Buswelu wilayani Ilemela.
Mtuhumiwa huyo Julai 14,2025 majira ya saa mbili usiku barabara ya Buswelu aliendesha gari namba T. 409 DTW aina ya
toyota harrier akiwa amelewa.
Wengine ni Deus Numbu(36),Mkazi wa jijini Dar-es-Salaam,ambaye Julai 18,2025, majira ya saa nane mchana Ilalila wilayani Ilemela,alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T. 666
DUC aina ya toyota land cruiser akiwa amelewa,Mwita Marwa(52),Fred Lukanga(71) na Nestory Oliva(40).
Huku wengine ni Abel Kiswaga(42),Japhet Njimbani(30),Hamza Rashid(54),James
Kalulema(42),Mwita Warioba(53),Peter Pamba(29) na Severine Ernest(47).

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina