December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ulega:Tuna matarajio ya kuona matokeo zaidi mkutano wa AGRF

Na David John timesmajira online

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema kuwa kazi kubwa inayofanywa na serikali kupitia Wizara yake ni kuvuta uwekezaji,mitaji,teknolojia za kisasa ,kufungua milango ya biashara huku akisema matarajio baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) nikupata uwekezaji zaidi.

Amesema kuwa shida waliyonayo wanataka kuwaingiza vijana na akina mama ili waweze kufanya uzalishaji wa mifugo ,lakini tatizo kubwa lililopo ni upatikanaji wa mitaji hivyo moja ya kazi ya mkutano huo ni kutafuta majibu na ndio maana kama Serikali wanasukuma hilo.

Waziri Ulega ameyasema haya Leo septemba 6 jijini Dar es salaam katika mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula ambao unafanyika kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere.

Amesema kuwa wao Kama Serikali wanajitajidi kusukuma lakini pia hata upande wa masoko pamoja na teknolojia za kisasa kwasababu Duniani watu wameshatoka siku nyingi  na Kuna utofauti mkubwa wa kufuga na ambavyo watanzania wanavyofanya biashara hivyo kujifunza mambo ni jambo jema ili Kubadilisha baadhi ya tamaduni zilizozoeleka.

“Kwa msingi huu mara baada ya mkutano huu tunafanya ufuatiliaji kupitia kamati maalumu ambazo zitafanya (forum ) ya mambo yote ambayo tunayapata kupitia mkutano huu ili kusudi isiwe tu mkutano na baada ya huu mkutano nini matarajio hivyo tutafanya ufuatiliaji.”Amesema Waziri Ulega 

Nakuongeza kuwa “Kwa Kila mkutano tuliofanya ,Kila mikataba tuliyosaini, Kila makubaliano tuliyofanya,tutaifanyia kazi Kwa maendeleo ya taifa letu ,watu,na Kwa maendeleo ya sekta ya mifugo na uvuvi.”amesisitiza Ulega

Akizungumzia malengo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  Waziri Ulega Amesema wanataka mikopo ya vijana ,na Akina mama ipelekewe zaidi kwenye sekta za uzalishaji ambayo inaongozwa na kilimo ,mifugo ,na uvuvi na  matarajio yao ni hayo ili kutoa kipaumbele zaidi kwenye upande huo.

Katika hatua nyingine Waziri Ulega Amesema katika mkutano maalumu wa Wizara yake wamezungumza kuhusu upatikanaji wa malisho na chini ya Wizara tatu wamezungumza Kwa pamoja, wamefanya makubaliano ya kuonyesha utayari wa Serikali kuonyesha jambo hilo linapatiwa ufumbuzi Kwa kulinda ng’ombe wasiendelee kufa kutokana na ukame.

pia amesema wazalishaji wakuku na wao wanapata wakati mkugumu sana hasa katika nyakati za kiangazi kwasababu ya upatikanaji finyu ñwa mahindi ambayo yanapanda bei  nakuongeza gharama za uzalishaji hivyo wamezungumzia hilo  Kwa pamoja.

“Serikali tumeonyesha utayari mkubwa ,wa kwamba namna gani sisi kama wasaidizi wa Rais wa Dkt Samia tulivyo tayari na kutatua changamoto ambazo zinakabili sekta zetu za uzalishaji nchini na hasa  katika kuyaleta makundi ya vijana na akina mama waweze kuzalisha.”Amesema Ulega .

Ameongeza kuwa kuhusu kuchanja Kwa wale wanaofanya ufugaji kibiashara wa mifugo uchanjani ni wa asilimia 100  na hata wengine wanafanya lakini Kwa wanaofanya ufugaji wa kawaida wa kiasili Kuna asilimia 20 hivyo kunahitajika kujitahidi kutoka huko.

Akizungumzia magonjwa ambayo wanakwenda kuyapa kipaumbele na ikumbukwe Kuna magonjwa takribani matano ,magonjwa ya midomo na miguu mwa ng’ombe,magonjwa ya mapafu ya ng’ombe na kondoo,magonjwa utupaji Mimba,mdondo, na magonjwa mengine na matarajio yao nikuazia mwezi 9,10 waweze kwenda kuaza kampeni hiyo.

Amefafanua kuwa BBT imetengwa Bilioni 20 Kwa ajili ya kuongeza vituo na hivi Sasa Mpango wao ni kushirikiana na mikoa nchini .kama Tabora , morogoro , wako tayari kuchukua jukumu nankwenda nalo huko ili kwenda kutengeneza miundombinu na Mwazo walioweka vituo nane ambavyo viko chini ya Wizara Moja Kwa Moja