Na Mwandishi wetu,Timesmajira Online
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amekabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu wilayani Mkuranga, mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuinua maendeleo ya sekta ya elimu wilayani humo.

Ulega amekabidhi vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika wilayani Mkuranga Februari 12, 2024.
Vifaa alivyokabidhi ni madaftari,viatu, mabegi na mashine za photocopy ambavyo vyote vimegharimu kiasi cha milioni 42 na kunufaisha wanafunzi takribani 300.
“Shukrani kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha elimu inawakomboa watanzania wote, ameboresha mpango wa elimu bure mpaka kidato cha sita na ametanua wigo wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya vyuo vikuu na vyuo vya kati ili kila kijana apate fursa ya kusoma,” amesema.

Pia, Waziri Ulega ametoa motisha kwa wanafunzi waliopata matokeo mazuri katika masomo yao ya kidato cha nne waliokuwa wanasoma katika shule zilizopo wilayani Mkuranga.

More Stories
Ngozi:Wanawake nchini wanakila sababu ya kumshukuru Rais Samia kutoa nafasi za uongozi kwao
Wataalamu wa ujenzi mfumo wa NeST wanolewa usalama wa mifumo
Mkurugenzi Rapha Group aeleza fursa mashindano Tulia Marathoni