Na Bakari Lulela,Timesmajira
CHAMA cha usanifu wa kiswahili na ushairi Tanzania (UKUTA) kimefanya mkutano mkuu jijini Dar es salaam, kwa kuweka mipango thabiti sambamba na wanachama kuridhia namna bora ya kuendesha zoezi la uchaguzi kwa kuwapata viongozi bora wenye weredi wa kukiongoza Chama hicho ambapo unaotarajia kufanyika Januari 2026.
Uchaguzi huo unatarajia kuwa wa kidemokrasia kwa kuendesha zoezi la upigaji kura kwa kufuata hatua za uwekaji alama ya ndio ama hapana kwenye kisanduku kwa wagombea watarajiwa kushiriki zoezi hilo akiwemo mwenyekiti, makamu wake, Katibu na makamu wake, mweka hazina na msaidizi wake pamoja na Katibu mwenezi.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa mkutano huo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Shekh Amiri Karutta amesema lengo la mkutano wetu ulikuwa ni kujadiliana na wanachama namna nzuri ya kuliemdea zoezi la uchaguzi wetu
” Uchaguzi huu utakuwa katika sura ya kipee kwa kufuata kidemokrasia kama ambavyo tulivyoendesha zoezi lililopita kwa kumchagua mgombea mmoja mmoja kwa kufuata akidi iliyopo ya wajumbe wa chama walio na sifa,” amesema Shekh Karutta

Aidha mkutano huo kulikuwa na burudani mbalimbali zilizotolewa kwa njia ya mashairi kutokana na wengi wa wanachama kuwa ni wabobezi wa Lugha ya kiswahili na ushairi ambapo dhima kubwa ni kuelekea uchaguzi mkuu wa kuchangua viongozi wa kukiendesha chama katika kipindi kijacho.
Kwa upande wake mwakilishi wa kutoka Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) anayehusika kusimamia sanaa za maonesho,Lilian amesema kuwa katika mchakato wa kuchangua viongozi wenu mnatakiwa kujiimalisha kwa kuhakikisha mnakuwa wamojaÂ
“Katibu mtendaji wa BASATA anawatakia uchaguzi wenye kheri ila anawasihi kujiimalisha kwa kulipa ama kuuhisha nyaraka zenu Ili uchaguzi wenu uende vizuri kwa amani na salama,”Amesema Lilian.
Ameendelea kusema kuwa viongozi watakaochaguliwa wawe na dira ya maendeleo ya kuongeza umoja huo ambapo jukumu la kuuongoza umoja wa washairi Tanzania utokane na viongozi watakaochaguliwa hivyo ni muhimu kuwa wamoja kwenye kufanya kazi za kijamii na Taifa kwa ujumla wake.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi