Na Penina Malundo,TimesMajira.Online
UKATILI wa Kijinsia ni miongoni mwa changamoto ambayo watu wanakumbana nazo ikiwemo kunyanyaswa, kupigwa, kutelekezwa na hata wale wanaowafanyiwa ngono bila ridhaa zao wengine wakiwa na umri mdogo.
Hellen Daniel ni miongoni mwa mzazi ambaye ambaye mtoto wake amekumbana na janga la kufanyiwa ukatili baada ya mume wake kukimbiwa ambaye alibahatika kuzaa nae watoto watatu.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuja Dar es Salaam kufanya kazi za ndani baadae kuingi kwenye mahusiano yaliyodumu kwa miaka mitatu lakini hali ilibadilika pale alipopata mtoto ambaye ana ulemavu wa miguu.
“Nilipojifungua tu mtoto wangu wa mwisho na kufahamu kuwa ni mlemavu mambo yalianza kubadilika sana, alikuwa akininyanyasa hata pesa ya chakula alikuwa haniachii na mwishowe hakurudi nyumbani.
“Kwa kweli nilipata shida sana,nilikuwa na maumivu katika moyo wangu kwa ukatili wa mume wangu alioufanya wa kunitelekeza …nilikuja kufukuzwa pale nilipokuwa nakaa na kwenda kupanga nyumba nyingine,”anasema.
Anaeleza baada ya mumewe kumkimbia hali ilikuwa tofauti alianza kupambana kutafuta pesa ili watoto wake wale kwa kufanya kazi ndogpo ndogo.
Judith Kimaro ni Afisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni ,anasema masuala ya ukatili wa kijinsia kwa Manispaa ya Kinondoni yapo ila sio mengi kama kipindi cha nyuma.
Huku akieleza kuwa kwa sasa changamoto kubwa ipo katika ukatili wa kihisia ,kimwili na ukatili wa kiuchumi wakati ukatili wa kingono ukionekana kupungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na kipindi cha miaka ya nyuma.
“Ukatili wa kijinsia unaoripotiwa kwa kasi sana sasa hivi ni ukatili wa kihisia na kimwili(kupigwa kwa watoto),watoto wengi wanakuwa wanabughudhiwa na wazazi wao au walezi wanaoishi nao,”anasema na kuongeza
“Kwa Kinondoni ukatili wa kijinsia umeonekana hasa katika kata ya Mwanyamala,Tandale,Ananasifu,Kigogo na Bunju,kata hizi zinaripoti sana masuala ya ukatili wa kijinsia,”anasema.
Afisa ustawi wa jamii huyo wa Manispaa ya Kinondoni anasema kwa mwaka wa fedha 2018/19 kuanzia Julai hadi Septemba takwimu zinaonyesha kuwa ukatili wa jinsia kwa upande wa kimwili(Vipigo,kuchomwa na kitu chenye ncha kali watoto wakike walikuwa 11 wakiume wakiwa 6.
Wakati ukatili wa Kihisia(kutukanwa) watoto wa kike ulikuwa 16, wakiume 9 jumla wakiwa 25, Ukatili wa Kingono (kubakwa,kulawitiwa) watoto wa kike walikuwa 9,wakiume 4 jumla 13,.
Ukatili wa Kiuchumi (Kunyimwa kwenda shule) watoto wakike walikuwa 19,wakiume 11 jumla 30,Jumla ya ukatili wa kijinsia waliofanyiwa watoto kipindi hicho wakike walikuwa 16, wa kiume 10 jumla26.
Na mwaka 2019/2020 katika miezi hiyo hiyo Julai hadi Septemba takwimu zinaonyesha kuwa ukatili wa kijinsia kwa upande wa kimwili (Vipigo,Kuchomwa na kitu chenye ncha kali )kwa watoto wa kike walikuwa 16, wakati kwa upande wa wanaume ulipungua mpaka asilimia 0 jumla 16 .
Kwa upande wa ukatili wa kihisia (Kutukanwa) watoto wa kike walikuwa 0 ,wakiume,7 Jumla ikiwa watoto 7,.
Vilevile ukatili wa Kingono ukishuka kutoka matukio 13 hadi matukio 8 (kubakwa,kulawitiwa ),watoto wa kike 5 na kiume 3 jumla 8 .
Huku ukatili wa kiuchumi (kunyimwa kufanya kazi, kwenda shule) watoto wakike uliongezeka takribani mara 10 zaidi mwaka 2019/2020 nakufikia 205, hivyo hivyo kwa watoto wakiume ukiongezeka mara 14 na kufikia matukio 156 ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto waliofanyiwa kipindi hicho.
Kwa Upande wake Mwakilishi wa Kituo cha Usuluhishi cha Huduma ya Ushauri na Nasaha ( CRC) kilichokuwa Chini ya Chama cha Waandishi wanawake (TAMWA),Gladness Munuo anasema wamekuwa wakipokea kesi mbalimbali zinazowakabili watu hususani zile za ukatili wa kijinsia wa watu kutelekezwa.
Anasema kituo chao kimekuwa kikisaidia kumaliza kesi mezani zinazowakabili watu mbalimbali kwa kufanya masuluhisho.
Ansema kesi kubwa zinazowafikia katika kituo hicho ni pamoja na wazazi upande mmoja kuwatelekeza watoto,Kesi za Ndoa pamoja na kesi za mirathi hususani kwa wanawake.
Munuo anasema ndani ya kipindi cha miaka 10 wameweza kufanikiwa kusuluhisha kesi nyingi huku zilizomalizika kabisa zikiwa kesi 25 tu.
Hali ikiwa hivyo ripoti ya Takwimu Muhimu za Tanzania mwaka 2019 (Tanzania in Figures 2019) ya Ofisi ya NBS imeeleza kuwa makosa ya ubakaji yameongezeka kwa asilimia 2.8 kufikia makosa 7,837 kutoka 7,617 kwa mwaka 2018.
Hivyo juhudi zaidi zinahitajika katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kutokana na tafiti mbalimbali kuonesha ongezeko la vitendo hivyo bado vinaendelea kufanyika katika baadhi ya maeneo.
More Stories
Siri ya Rais Samia kutembea kifua mbelea kijivunia Mapinduzi Matukufu ya Z,bar
Rais Samia anavyotimiza ahadi yake ya kumtua ndoo ya maji mwanamke
Rais Samia anavyozidi kusogeza karibu watoto wa kike na kasi ukuaji teknolojia