January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ujenzi wa Hospitali ya rangitatu wafikia asilimia 69

Na Prona Mumwi,Timesmajira

Ujenzi wa hospitali ya rangitatu iliyopo Mkoa wa Dar es salaam wilaya ya Temeke umefikia asilimia 69 na hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bilioni 10.8.

Fedha hizo ambazo zimetolewa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania,Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Afya na Manispaa ya Temeke kwa kupitia mapato ya ndani na unatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa sita.

Ujenzi huo wa hospitali ya kisasa unatarajiwa kuwa mkombozi kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake kwa kupata huduma za kiafya za kibingwa kutoka kwa madaktari wabobezi.

Ujenzi wa jengo la ghorofa Sita la Hospitali ya Mbagala Rangi lengo kuu ni kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za afya na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika kupata huduma za kutabibu kwa umbali mrefu na kushindwa kufanya shughuli za kujiletea maendeleo.

Aidha Hospitali hiyo iliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mkoani Dar es Salaam ambapo Rais Dkt. Samia katoa Bilioni Mbili na Wizara ya Afya imetoa Bilioni Mbili pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wametenga Bilioni Mbili kwa hiyo na fedha nyingine ni kutoka benki ya dunia.

Hata ivyo watendaji wa Wilaya hiyo wametakiwa kuhakikisha wanatafuta maeneo ya kujenga majengo ya huduma za Afya ili kuwapunguzia wananchi changamoto ya msongamano wa kupata huduma.

Ujenzi huo wa hospitali ya kisasa unatekelezwa na Kampuni ya Kichina ya group six ltd na unatarajiwa kukamilika kwa wakati.