November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ujenzi kituo cha kupokea,kupoza umeme wafikia asilimia 50

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

Serikali, imesema inaendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini,huku  utekelezaji wa  mradi wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza  umeme kilichopo Tunduru, umefikia asilimia 50.

Hayo yamebainishwa Septemba  28,2024,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia  Suluhu Hassan,wakati akihitimisha ziara yake mkoani Ruvuma, iliolenga  kujipima ni kiasi gani Serikali,imeweza kutekeleza ahadi ilizo zitoa kwa wananchi.

“Kukamilika kwa mradi huu pamoja na kuunufaisha Mkoa wa Ruvuma,pia utaunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara  kuiwezesha kupata umeme wa gridi ya Taifa,”amesema  Dkt.Samia na kuongeza:

“Serikali inafanya juhudi kubwa, katika kusogeza huduma za umeme kwenye kila kijiji,ambapo kupitia REA, imefikisha umeme kwenye vijiji 541 kati ya vijiji 551 vya Mkoa wa Ruvuma,na inaendelea kusogeza huduma kwenye vitongoji mkoani humo,”.

Pia, ametoa wito kwa wananchi ambao bado hawajalipwa fidia,kupisha mradi huo  wa  umeme ili uendelee na utekelezaji wake.Huku akisisitiza kuwa Serikali italipa fidia zao,na  hakuna mwananchi ambaye hata lipwa fidia.

Sanjari na hayo,amewataka viongozi  wa Serikali na watumishi,kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, ili kuokoa maisha ya watanzania pamoja na misitu.