January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ujenzi kituo cha afya Zingiziwa wapongezwa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalah Shaib Kaim, amepongeza ujenzi wa mradi wa kituo cha Afya Zingiziwa wilayani Ilala ambao umegharimu shilingi Milioni 636.5

Akitoa pongezi hizo wakati wa kuzindua Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Ilala Abdalah Shaib Kaim, alianza kwa kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuipatia Halmashauri pesa kwa ajili ya miradi ya vituo vya Afya .

“Nimelidhishwa na mradi huu Kituo cha Afya Zingiziwa kituo cha Afya cha kisasa wananchi waweze kutumia kituo cha Afya chao ambacho kimejengwa na Serikali napongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji ,Meya Omary Kumbilamoto na Mganga Mkuu Dkt.Eldhabeth Mnyema ,Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo kwa usimamizi mzuri katika miradi hii ya Serikali ” alisema Shaib .

Aliwataka Wananchi kutumia miradi ya Serikali vizuri na kuitunza Ili iweze kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo .

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt .Eldhabeth Mnyema alisema mradi wa kituo cha Afya Zingiziwa ulianza February 2022 mradi unatekelezwa kwa kutumia force akaunti chini ya usimamizi wa Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji na kamati za ujenzi za Kituo .

Dkt,Edhabeth alisema fedha zilizopokelewa ni shilingi 575,000,000 mapato ya ndani mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 547.3 zimetumika katika ujenzi jengo la wagonjwa wa nje (OPD) milioni 192 mahabara shilingi milioni 119.8 jengo la Wazazi milioni 176 .2 na Jengo la upasuaji shilingi milioni 59.1 .

Aidha alisema mpaka sasa mradi umefikia asilimia 95 ya Utekelezaji na unategemewa kukamilika Juni 30/2023

Mwenge wa uhuru ulizindua miradi sita ya Maendeleo Wilaya ya Ilala yenye thamani ya shilingi 17,359,411,606.41 ambayo yote ilizinduliwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ikiwemo miradi ya Barabara ,Sekta ya Elimu ,Afya,Mazingira,Maji,na kikundi cha Vijana cha utengezaji vikoi .