November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Helen Whately. (Picha na Mtandao).

Uingereza yawataka wananchi kula kidogo kuepuka vifo dhidi ya Corona

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, London

Serikali ya Uingereza leo inatarajia kuweka zuio la matangazo ya vyakula vyenye mafuta, sukari na chumvi kupitia runinga na mitandaoni ikiwa ni hatua ya kudhibiti ulaji ambao unasababisha kunenepeana ovyo, hivyo kuhatarisha afya za wananchi dhidi ya virusi vya Corona (COVID-19).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya leo, Helen Whately ikiwa ni hatua moja wapo ya kuwafanya Waingereza kula vyakula kidogo, kwani ulaji zaidi umetajwa kuwaweka wengi hatarini dhidi ya corona.

Kwa mujibu wa Reuters, Waziri Whately amesema, watu wengi wenye uzito kupindukia wapo hatarini zaidi kufa kwa virusi vya corona nchini humo.

Uingereza pia inazuia matangazo ya vyakula visivyo vya kawaida, kwani kwa sasa mawaziri wanatafuta njia mbalimbali za kudhibiti shida ya ugonjwa wa kunenepena sana nchini humo.