Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Tarehe 24.02.2022 muda wa saa 4:00 asubuhi huko maeneo ya Sakina katika Halmashuri ya Jiji la Arusha askari wa jeshi la akiba (mgambo) waliwakamata Ester Jackson (38) na Isaya Mollel (20) wote wakazi wa Ngaramtoni wakiwa na Bhangi misokoto 1755 na kuwafikisha katika kituo kidogo cha Polisi Sakina.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya watu waliwasiliana na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambapo walifika eneo la tukio na kuanza kufanya mahojiano na baadhi ya wananchi ambao walishuhudia tukio hilo. Wakati waandishi hao wakiendelea kuwahoji watu katika eneo la Raskazoni, askari
mgambo hao walipita katika eneo hilo. Inadaiwa waandishi hao waliwasimamisha kwa
lengo la kuwahoji, kitendo hicho pamoja na kupigwa picha kiliibua mzozo kati ya waandishi hao na mgambo.
Waliendelea kuvutana kuanzia eneo la Raskazoni hadi eneo la Sakina kilipo kituo cha Polisi na kusababisha vurugu eneo hilo. Askari polisi waliokuwa zamu katika kituo hicho waliomba msaada kutoka kituo cha Polisi kati (Central), kutokana na idadi ya watu kuanza kuongezeka katika kituo hicho, Mkuu wa kituo cha Polisi Kati alifika kituoni hapo na kuwachukua waandishi hao wa habari pamoja na mgambo kwa ajili ya mahojiano, ambapo waliachiwa baada ya kuhojiwa.
Baada ya kupata maelezo ya watu mbalimbali walioshuhudia kuanzia chanzo cha mzozo huo, jalada litapelekwa kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa maamuzi ya kisheria.
Jeshi la Polisi Mkoani hapa litaendelea kuhakikisha wananchi wakiwepo waandishi wa habari wanaendelea kufanya shughuli zao katika mazingira ya amani, utulivu na usalama kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.
JUSTINE MASEJO-ACP
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA ARUSHA
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba