November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UDSM yaja na gari la umeme maonesho ya Vyuo Vikuu

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam.

MKUU wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (UDSM) Dkt. Dotto Kuhenga, amewataka wananchi hususani, wanafunzi waliomaliza kidato cha sita, kutembelea katika banda la chuo hicho, lililopo katika maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu, yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini hapa.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dotto Kuhenga.

Ambapo ameeleza kuwa katika maoesho hayo ipo miradi mbalimbali ambayo wanaonesha kwa wananchi watakaofika katika banda hilo ikiwa ni pamoja na mradi wa uwatamizi (Incubator) uliogunduliwa na wanafunzi wa chuo hicho pamoja na mradi wa gari la umeme lililotengenezwa na andaki la chuo hicho la uhandisi na teknolojia.

Maonesho hayo ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yamefunguliwa rasmi jana na Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda, huku yakisindikizwa na kauli mbiu ya “Kukuza ujuzi nchini kupitia elimu ya juu sayansi na teknolojia kwa uchumi imara na shindani”.

Akiongea na waandishi wa habari katika maonesho hayo, Dkt. kuhenga amesema, hadi sasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kinatoa kozi zaidi ya 130 kwa upande wa shahada ya awali kati ya kozi hizo ni za masuala ya sayansi, udaktari wa binadamu, sheria, uandishi wa habari, sanaa,uhandisi na nyingine nyingi.

“Chuo chetu cha UDSM tunatoa kozi mbalimbali,kushiriki katika maonesho haya tunaamini hapa tunakutana na watu mbalimbali, hususani wanafunzi waliomaliza kidato cha sita,”.

Aidha ametoa wito kwa wahitimu wa elimu ya juu kutokuwa na desturi ya kutegemea kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo yao, bali wawe na utaratibu wa kujiajiri ili kujiingizia kipato pindi nawapokuwa wanasubiri ajira pale zitakapotoka.

Maonesho hayo, yalianza Julai 17 na kufunguliwa rasmi na Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda Jana na kutarajiwa kumalizika Julai 22 mwaka huu.