March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UDSM yabuni teknolojia mpya ya kuhesabu Samaki

📍 Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online – Dodoma

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia wataalamu wake wa maabara kimebuni mashine mpya ya kisasa ya kuhesabu samaki kwa njia ya kiotomatiki (automated fish counting system), ikiwa ni mara ya kwanza kwa teknolojia hiyo kutumika nchini Tanzana.

Ubunifu huo unaonyeshwa katika Maonesho ya Nanenane, ukilenga kuongeza ufanisi na tija kwa wafugaji wa samaki kote nchini.

Akizungumza katika maonyesho ya wakulima na Wafugaji,Mbunifu wa mashine hiyo Mwanasayansi wa Maabara Kutoka UDSM Ditram Ngairo amesema mashine hiyo ni nyenzo Bora na rahisi katika kujua idadi ya samaki katika mabwawa


Mashine hiyo imewasilishwa kwa mara ya kwanza kwenye Maonesho ya Kilimo ya Nanenane, yanayofanyika Dodoma mwaka huu, kama sehemu ya kuonesha mbinu bora za kisasa za kuongeza tija katika ufugaji wa samaki.

Ngairo amesema mashine hiyo imebuni baada ya utafiti wa kina kufanywa kuhusu changamoto zinazowakabili wafugaji wa samaki nchini Tanzania hasa katika kujua idadi yao.

Amesema kwa muda mrefu, wafugaji wa samaki walikuwa wakitegemea njia za jadi kama kupima au kuhesabu samaki kwa mikono njia ambazo si sahihi, ni ngumu na zinazosababisha vifo vya samaki kutokana na mfadhaiko.

Amesema mashine hii ya kuhesabu kwa njia ya kiotomatiki inapunguza muda wa kuhesabu, hupunguza vifo vya samaki, huongeza ustawi wa samaki na hivyo kuchangia ukuaji wao wa haraka. Pia husaidia katika biashara kwa kuhakikisha mnunuzi analipia idadi halisi ya samaki bila kudhulumiwa.

.