March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UDSM YABUNI TEKNOLOJIA MPYA KUWEZESHA WAKULIMA KUPATA HUDUMA ZA KILIMO KIRAHISI

Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Uhandisi Kilimo, Vicent Tsoray akionyesha Teknolojia ambayo humwezeshakulima kuwasiliana na kupata huduma ya zana za kilimo

l

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kupitia Idara ya Uhandisi Kilimo, kimekuja teknolojia mpya kwa njia ya application ya simu janja itakayowawezesha wakulima kupata huduma za kilimo na vifaa muhimu kutoka kwa watoa huduma kwa urahisi na haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya wakulima na Wafugaji jijini Dodoma katika viwanja vya Nzuguni , Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Uhandisi Kilimo, Vicent Tsoray amesema kuwa teknolojia hiyo inalenga kuboresha kilimo nchini kwa kuunganisha wakulima na watoa huduma wa zana na mashine za kisasa za kilimo kama vile matrakteta (tractors), mashine za kuvunia mazao (harvesters), pamoja na vifaa vya kunyunyizia dawa na mbolea mashambani.

โ€œApplication hii ina sehemu mbili kuu โ€“ moja kwa wakulima na nyingine kwa watoa huduma wa zana za kilimo. Mtumiaji atajisajili kwa kuweka jina na nywila, na kisha kuchagua upande wake kama mkulima au mtoa huduma,โ€ amesema Vicente.

Katika kueleza namna mfumo huo unavyofanya kazi, Mhadhiri huyo alibainisha kuwa mkulima ataanza kwa kuchagua huduma anayohitaji, pamoja na kueleza ukubwa wa shamba lake na aina ya zao analolima. Mfumo huo utamuonesha orodha ya watoa huduma waliopo karibu na aina ya huduma wanazotoa. Mtoa huduma atakapopokea taarifa hiyo, mfumo utaelekeza hatua kwa hatua jinsi huduma hiyo itakavyotolewa.

Kwa mujibu wa Vicent, teknolojia hiyo inalenga kupunguza changamoto za upatikanaji wa vifaa vya kilimo, kuokoa muda wa wakulima na kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo nchini.

โ€œTumeona kuwa wakulima wengi wanakosa zana kwa wakati au hupata huduma kwa gharama kubwa. Kupitia teknolojia hii, tunaleta mapinduzi katika sekta ya kilimo kwa kutumia mifumo ya kidigitali,โ€ ameongeza.

Teknolojia hiyo imebuniwa na watafiti wa UDSM kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, na inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kwa matumizi ya wakulima wa vijijini na mijini katika kipindi kifupi kijacho.