Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo bora, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, wamekabidhi matundu 13 ya choo katika shule ya msingi Changanyikeni kama sehemu ya kutekeleza mikakati yake ya kuifikia jamii.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo jana Jijini Dar es Salaam, Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye ameagiza kufanyike maboresho katika shule hiyo ikiwemo kuweka uzio ili kuongeza umakini kwa wanafunzi katika kujifunza.
“Ukiangalia mazingira na nilipotoka wiki mbili zilizopita, mazingira siyo mazuri sana , ukiangalia shule za wenzetu huwezi kulinganisha na hapa, hali niliyoiona sijafirahishwa nayo sana, ingawa tuna choo kizuri lakini kina picha tofauti na maeneo mengine ya hapa shuleni”
“Pesa mnazopata kila mwezi tuifanye mpango wa kubadilisha mazingira haya kwa kuweka ukuta kwani kuna muingiliano wa makazi ya watu na shule, kila mtu anapita anavyotaka , hii itavunja usikivu wa wanafunzi wetu watashindwa kujifunza”
“Hatakama siyo leo au kesho, tunahitaji
Kufanya zaidi ya hiki choo, madarasa ya shule ya awahi hali si nzuri, wanapopikia chakula cha wanafunzi
Pia mazingira si mazuri na ni padogo, hali itakapokuwa nzuri basi tujenge hata banda kubwa la kupikia” Aliongeza
Prof. Anangisye aliendelea kwa kusisitiza kwamba uwekaji wa mazingira bora shuleni hapo kutaendelea kuweka alama nzuri katika chuo kikuu cha Dar es Saam.
“Sisi kama chuo
Kikuu cha Dar es salaam mfikirie tusiishie
Kwenye choo bali tuangalie jinsi gani tutafanya tena kwani mazingira si mazuri, picha ya shule hii ndiyo picha ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ningetamani sana shule zetu ( Msewe ma Changanyikeni) zioneshe kwamba kuna chuo kikuu kikongwe katika nchi hii”
Aidha amesema Chuo
Kitaendelea kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto zinazozikabili jamii kwa kufundisha tafiti na kutuoa huduma kwa jamii
“Yanapotokea maafa tunawajibika, popote tunaposikia kuna lolote linawapata watanzania wenzetu tunakua mstari wa mbele kuhakikisha kwamba kile ambacho tumekipata tunakitumia
Kwenda kuwafikia hao”
Kwa upande wake Afisa Elimu Manispaa ya kinondoni,Mtundi nyamuhangwa,amekipongeza chuo kikuu kwa msaada wa ujenzi wa vyoo hivyo kwani vitasaidia kutatua changamoto zilizopo chuoni hapo ya kuwa na matundu machache ya choo.
Pia Nyamuhangwa,ameahidi kwamba watakitunza choo hicho ili kiendelee kuwa bora zaidi kwa matumizi ya sasa na hapo baadaye.
More Stories
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?
Watendaji Songwe wapatiwa mafunzo uboreshaji daftari la mpiga kura
Samia: Mwaka 2024 ulikuwa wa mafanikio