Na David John, TimesMajira Online
DAU nono la udhamini lililotolewa na kampuni ya Azam kuelekea msimu ujao kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara limewaongenea ‘mzuka’ mabingwa wa Ligi Daraja la Pili (SDL), Green Worrious ambao wamejitapa kufanya usajili makini ili kuweza kufanya vizuri katika msimu mpya wa Ligi Daraja la kwanza (FDL) na kisha ligi kuu.
May 25, mwaka huu Azam Media ilitangaza udhamini wa Sh. bilioni 225.6 wa haki ya matangazo ya televisheni kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo katika udhamini huo wa miaka 10 kuanzia msimu wa 2021/2022, asilimia 67 ya pesa itakuwa malipo ya kila msimu kwa klabu ambapo Azam itatoa Sh. bilioni 12 ambapo nane zitaelekezwa kwa klabu huku bilioni nne zikielekezwa kwenye maendeleo ya soka, shirikisho la Soka Nchini (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).
Fedha hizo zitaendelea kuongezeka kwa kila msimu na msimu wa mwisho wa mkataba yaani Azam itatoa bilioni 28 ambapo timu zote kwa ujumla zitapata takribani bilioni 19 huku bingwa kuanzia msimu ujao wa 2021/22 mpaka msimu wa 2023/24, ataondoka na kitita cha Shilingi milioni 500 kwa msimu huku dai hilo likiongezeka hadi Sh. milioni 700 kwa msimu wa 2028/29 hadi 2030/31.
Katika misimu mitatu ya kwanza mshindi wa pili ataondoka na Sh. milioni 250, mshindi wa tatu atapata Sh. milioni 225 huku mshindi wa nne akiondoka na Sh. milioni 200 na fedha hizo zitakuwa zikiongezeka kila msimu kwani hadi kufikia 2028/29 hadi 2030/31 bingwa atakuwa akipata Sh. milioni 700, mshindi wa pili ataondoka na Sh.milioni 325, mshindi wa tatu milioni 275 wakati mshindi wa nne atabeba Sh. milioni 250.
Pia kuanzia msimu ujao hadi 2023/24 mshindi wa tano ataondoka na milioni 65, milioni 60 na watakuwa wanadizidiana milioni 5 hadi kwa msindi wa 13 ambaye ataondoka na Sh. milioni 25 huku timu zitakazocheza hatua ya mtoano zikiondoka na milioni 20.
Kwa msimu wa 2028/29 hadi 2030,31 mshindi wa tano ataondoka na milioni 140 na watakuwa wakizidiana kiasi cha Sh. milioni 10 hadi mshindi wa 13 atakayeondoka na milioni 60 wakati timu zitakazocheza hatua hatua ya mtoani zikiondoka na milioni 50.
Akizungumza na Mtandao huu, msemaji wa mabingwa hao wa SDL ambao waliwahi kuitoa Simba Kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la Azam, Willam Kulwa amesema, wamejipanga vizuri kuhakikisha wanakwenda kufanya makubwa katika michuano ya FDL ili kupanda hadi ligi Kuu na kuvuna fedha za Azam.
Katika kuhakikisha ndoto za kucheza ligi hiyo inatimia, wanataka kufanya usajili wa nguvu ikiwa pamoja na kuimalisha bechi lao la ufundi ili kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zao za ambako kutawapa fursa ya kucheza ligi kuu misimu ijayo.
Amesema kuwa, kile walichokifanya katika SDL ndicho ambacho wanakwenda kukifanya FDL na kama alivyosema lengo ni kuona timu hiyo inapanda ligi kuu na watahakikisha hilo linafanikiwa kwa kushinda kila mchezo utakaokuja mbele yao.
“Hadi sasa tumefanya usajili wa kutisha na nyote mnakumbuka kazi kubwa aliyowahi kufanya Shabani Ndihile akiwa na timu yetu ya Taifa, hivyo sasa atakuwa akiwanoa makipa wetu lakini pia tupo mbioni kuanza usajili ambao utatuhakikishia kupanda haraka sana Ligi Kuu,” amesema Kulwa.
Amesema, hivi sasa watu wa Kinondoni wanapata raha kutokana na timu yao ya KMC kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu hivyo hata wao mashabiki wao kutoka Wilayani humo wakae mkao wa kula kutokana na timu hiyo ya Green Worrious kuonyesha nia ya kucheza ligi kuu.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania