March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uchaguzi Viti Maalum ,Wawakilishi,Ng’wasi ,Magufuli,Bulembo,Suluhu waibuka kidedea

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umekamilika kwa mafanikio, huku kura za uchaguzi wa wawakilishi wa vijana katika nafasi mbalimbali za Viti Maalum zikipigwa kwa amani na utulivu.

Kwa upande wa Tanzania Bara, jumla ya wagombea 31 walishiriki katika kinyang’anyiro cha nafasi nne za ubunge wa Viti Maalum. Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati Kuu, Mohamed Aboud Mohamed, jumla ya kura 2,466 zilipigwa, ambapo kura 12 ziliharibika na hivyo kura halali kuwa 2,454.

Akitangaza washindi kwa mwingi wa kura ,Msimamizi wa uchaguzi huo Mohames Aboud Mohamed amesema “Ng’wasi Kamani  kura 409,Jesca  Magufuli kura 391,Halima Abdallah Bulembo kura 320,Lulu  Mwacha  kura 316.

Kwa upande wa wabunge wa viti Maalum kupitia vijana  Zanzibar amesema  kura zilizopigwa ni 1,652, ambapo kura 8 ziliharibika na 1,644 zilihesabiwa kuwa halali ambapo amewataka wagombea waliopita kura nyingi ni Mwanaenzi Suluhu Hassan – kura 399,Latifa Khamis Juakali – kura 357,Zainab Bdalalah Issa kura 334 na Amina Ali Mzee aliyepata  kura 151

Aidha, katika uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa nafasi za Viti Maalum kundi la vijana Zanzibar, Salha Muhammed Mwinjuma aliibuka mshindi kwa kupata kura 255, akifuatiwa na Hudhaima Mbarak Tahir aliyepata kura 235.

Mkutano huu umetajwa kuwa wa kihistoria kwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu, ushiriki mkubwa wa vijana, na kuendelea kuimarisha demokrasia ndani ya UVCCM na Chama kwa ujumla.