April 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ubovu wa barabara mlima Kilimanjaro, changamoto watalii kufikia vivutio vya utalii

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online Dodoma

MBUNGE wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi amehoji mkakati wa Serikali wa kupanua wigo wa maeneo mapya ya utalii nchini.

Aidha katika.maawali yake ya nyongeza Bungeni jijini Dodoma Leo April 9,2025,Prof.Ndakidemi ametaka kujua kama Serikali haioni umuhimu kutumia pesa zinazotolewa kwa jamii inayozunguka mlima Kilimanjaro ama CSR kufanya ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami.

“Moja ya changamoto kubwa inayowakabili watalii kupanda mlima Kilimanjaro hadi kufikia vivutio vya utalii ni ubovu wa barabara,sehemu mbovu sana ni sehemu ya kata ya mbokomi inayopeleka watalii kuona mti mrefu kuliko yote Afrika na barabara ya Umbwe ambayo inapeleka watalii kwenda mlimani

“Kwa kuwa Kuna wingi wa kazi upande wa tarura je Serikali haioni umuhimu kutumia pesa zinazotolewa kwa jamii inayozunguka mlima Kilimanjaro ama CSR kufanya ukarabati wa barabara kwa kiwango Cha lami?

jPia alihoji “je wananchi wa kata ya Urushimbwe wamekuwa na kiu kubwa ya kujengewa lango la kuingia mlima Kilimanjaro kupitia katika kata hiyo Ili wananchi wapate ajira,je Serikali Ina mkakati gani wa kuwasaidia wananchi hao kupata lango hilo?

Akijibu maswali hayo,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Danstan Kitandula.amesema Serikali kupitia Kinapa imekuwa na utaratibu wa kukarabati barabara hizo zinazopeleka watalii kwenye maeneo ya vivutio vya utalii huku akisema,aserikali itaendelea kufanya shughuli hizo.

Aidha amesema , Serikali itahakikisha inatenga fedha za kutosha Ili kuhakikisha Wakala wa Barabara za mijini na Vijijini (TARURA) nayo inatekeleza majukumu yake.

Katika majibu yake ya swali la msingi,Kitandula.amesema ,
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kupanua wigo wa mazao ya utalii nchini kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi, kuongeza siku za kukaa kwa watalii, kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii, na kupunguza utegemezi katika zao la utalii wa wanyamapori.

Amesema,Mikakati hiyo inahusisha hatua kadhaa muhimu zinazolenga kuboresha na kupanua sekta ya utalii.

Kitandula.amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, Wizara imebaini vivutio vipya vya utalii 337 katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, na Kigoma. Zoezi hili la kubaini vivutio vipya linapangwa kuwa endelevu ili kuhakikisha kuwa maeneo mapya ya utalii yanagunduliwa na kuendelezwa.

Pia, Serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi ili kuendeleza mazao ya utalii ya kimkakati.

“Huu ni mkakati muhimu unaolenga kuongeza vivutio vya utalii kama vile utalii wa fukwe, meli, mikutano na matukio, malikale, utamaduni, na michezo. Kwa mfano, katika kuendeleza utalii wa meli nchini, Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau kutoka sekta binafsi, hasa wale wenye mtandao mkubwa katika soko la kimataifa la utalii wa meli, kutangaza na kukuza soko hili.” amesema Kitandula.na kuongeza kuwa

“Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, meli 9 za kitalii ziliwasili nchini, zikileta jumla ya watalii 2,944 ambao walitembelea vivutio mbalimbali vya utalii. Huu ni ushahidi wa mafanikio ya mikakati ya Serikali katika kuboresha na kupanua wigo wa utalii nchini.”