January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ubalozi wa Ufaransa nchini waanda tamasha la marafiki

Na David John,TimesMajira Online,Dar

KITUO cha Utamaduni cha Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kimeandaa tamasha la marafiki ambapo jumla ya bendi 16 na wasanii 128 watatumbuiza kwenye tamasha hilo la marafiki 2021.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye kituo cha utamaduni cha Ufaransa Allience francases mratibu wa tamasha hilo Isack Abeneko amesema marafiki ni tamasha la muziki la kimataifa ambalo huwaleta pamoja wasanii.

Mwanamuziki Akoth Jumadi kushoto,kutoka Kenya akitumbuiza katika utambulisho wa uwepo wa tamasha la marafiki.

Amesema katika tamasha hilo wasanii wa ndani na wakimataifa watapata fursa ya kuonyesha muziki wao ambapo pamoja na mambo mengine tamasha hilo litawaleta wadau pamoja na watalaamu mbaalimbali wasanaa na watashiriki pamoja na kubadilishana uzoefu.

“lengo la tamasha hili la marafiki nikuwajengea uwezo wasanii katika maeneo mbalimbali ya sanaa zao tamasha la marafiki linatarajia kuleta muziki mzuri wa moja kwa moja na maarifa kwa wakati mmoja kuanzia Oktoba 7,hadi 9 ambapo pia kutakuwa na marafiki extra firefly Bagamoyo Oktoba 10 “amesema Abeneko.

Kauli mbiu ya tamasha hilo ni ‘Muziki wa Maendeleo ya Jamii’ kuhamasisha vijana na wanamuziki kutumia muziki kama nyezo ya kuleta mabadikiko chanya ya kijamiii.

Mwakishi wa Katibu Mtendaji kutoka BASATA, Ibrahim Ibengwe (kulia) akizungumzia tamasha la marafiki

Pia tamasha la marafiki litakuwa na semina za mafunzo na mijadala ya wazi kwa siku tatu ambapo mada kama uratibu wa biashara ya muziki, utengenezaji wa muziki kwenye mzunguko na unaofaa kwenye usimamizi wa wasanii, jinsi ya kupata shoo katika soko la ndani na la kimataifa. Pamoja na jinsi ya Luanda epk zote zitawasilishwa.

Amesema mjadala wa wazi ukuwa juu ya biashara ya muziki na jinsi ya kuufanya muziki wa afro -fusion uwe muhimu na utumike ndani ya soko la Tanzania na afrika mashariiki nakwamba washa zitaaza saa 04:00 asubuhi 07 mchana siku zote tatu na zitafanyika Nafasi art space na Alliance Francaise .upanga Dar es salaam..

Ameongeza kuwa wasaniiii mameneja, wasimamizi wa sanaa, waandaaji, matamasha na wadau wa sanaa nakwamba wanaamini semina ya mafunzo ya biashara ya muziki ni jambo muhimu kwa waaasanii wote, wasimamizi, wa muziki, wandaji,wa matamasha na mameneja kujifunza na kukuza taaluma zao.

Mmoja wa ofisa kutoka kituo cha utamaduni cha Ufaransa .Alliance Francoise Soumeya Djafaar akizungumzia tamasha hilo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani

Moja ya wasanii watakao kuwepo ni pamoja na Akoth Jumadi kutoka kenya ,Bahati Female Band, Balaa Mc, Dabo Mtanzania, Iju Music, Justine Kaozya,wengeni ni Kudra Mazongela, Nasibo, Muteze, Sinaubi Zawose, StoneTown Rockerz ,Tarajazz Zanzibar, Tofa boy, Voice of Revolution Band, Witiri Tz, Zanubuntu pamoja na Ziad Daroueche.

Tamasha hilo pia limepata baraka Za Baraza la Sanaa Nchini (BASATA) ambapo mmoja wa watendaji wa baraza hilo Ibrahim Ibengwe alisema wao wamebarini huku wakitaka wadau kuunga mkono matamasha hayo kwa kutoa ufadhili.