October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

U-17 kujazwa milioni 34

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Saidia Ushindi ya Taifa Stars imeahidi kutoa dola za Kimarekani 15,000 ambazo ni zaidi ya Sh. milioni 34 kwa timu ya Taifa ya Wasichana chini ya umri wa miaka 17 ‘Tanzanite’ ikiwa watatwaa ubingwa wa michuano ya COSAFA.

Timu hiyo imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa goli 10-1 katika mchezo wao wa juzi dhidi ya timu ya Taifa ya Zimbabwe.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Cliford Ndimbo iliweka wazi kuwa, ikiwa timu hiyo itakabidiwa kitita hicho ikiwa watafanikiwa kuibuka na ushindi katyika mchezo wa fainali utakaochezwa Novemba 14.