November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tuzo za vijana Jumuhiya ya Afrika Mashariki Kuhamasisha kujiinua kiuchumi

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Waandaaji wa tuzo za vijana Jumuhiya ya Africa Mashariki wameziomba Serikali zote Saba za Jumuhiya ya Afrika Mashariki na sekretarieti yake pamoja na wadau mbalimbali kuwashika mkono ili kwa pamoja waweze kuondoa changamoto ya kutokuwa na ajira kwa vijana.

Wito huo umetolewa na Spika Mstaafu wa Bunge la vijana Jumuhiya ya Afrika Mashariki, Helena Mollel ambaye pia ni Muandaaji wa Tuzo za vijana Jumuhiya ya Afrika Mashariki (East Africa Youth Awards) zilizopo chini ya Taasisi ya East Africa Youth Foundation.

“Kilichonipelekea kuanzisha tuzo hizi ni kilio Cha vijana wengi kilikuwa ni ajira kwahiyo kupitia platfum hii hatutoi tu mipenyo ya jinsi ya kupata ajira lakini tunatoa pia fursa za kibiashara ambazo zipo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Vijana wakiona vijana wenzao wamepewa tuzo kwenye madini, utalii, afya ya uzazi n.k inawapa hamasa ya kuona kuna faida ya wao kuingia kwenda kuzifanyia kazi”

“Wito wangu kwa serikali zote 7 Jumuhiya ya Afrika Mashariki na sekretarieti ambayo tumeendelea kufanya nao kazi na wadau mbalimbali tunawaomba watushike mkono ili kwa pamoja tuweze kuondoa gepu la kutokuwa na ajira kwa vijana” Amesema Helena

Amesema Tuzo wanazozitoa kwa vijana zinalenga kuwapa hamasa katika Sekta tofauti tofauti kwenye kujiiunua na kujikwamua kiuchumi lakini pia kuendeleza mlengo wa secretariet ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kufanya nchi zote 7 zikawa Moja.

“Tunatoa tuzo ili tueneze nguvu ya vijana kuwa na hamasa ya kukubali kuwa na Muungano wa nchi zote 7 ili tuendee kwenye Jumuhiya Moja ambayo tunaweza kufanya biashara, kufahamiana na kumiliki ardhi bila ya kuwa na vizuizi vyovyote”

Aidha amesema umri muongozo wa Afrika Mashariki ni miaka 15- 35 ambapo kila siku kumwekuwa na ongezeko la vijana wanachipukia hivyo wanaendelea kutoa tuzo hizo ambazo hutolewa kwa mwaka mara moja na ambapo kwa mwaka huu 2023 ndiyo zimeanza.

“Vijana ndiyo wenye idadi kubwa Afrika Mashariki, kwahiyo tukiwapa tuzo vijana inakuwa ni njia ya wao kuungana, kufahamiana na kupata nafasi ya kufanya biashara zao nje ya mipaka yao ya nchi zao husika ambazo ziko ndani ya Afrika Mashariki”

“Tuzo hizi kwa mwaka zinafanyika mara moja tu, na zinashirikisha nchi zote 7 hivyo tunakuwa na michakato ya kutafuta vijana ambao tunaona wanafanya mambo makubwa kwenye nchi zao na kuwaleta katika sportlight ya Afrika Mashariki”

Amesema tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo mwaka huu, muitikio umekuwa mkubwa na wanaamini kwa miaka inayoendelea muitikio utakua mkubwa zaidi.

“Hii inatokana na sisi kufanya matangazo mengi zaidi hivyo tunatamani kwa mwaka 2024 tupate wadhamini wakubwa ambao wanaweza wakatifikisha sehemu mbalimbali za nchi zetu za Jumuhiya ya Afrika mashariku”

Kuhusu tuzo za heshima ambazo wamezitoa mwaka huu, Helena amesema tuzo ya kwanza vijana wa Afrika Mashariki wamemtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwasababu ametengeneza diplomasia ya nchi na ikasimama, lakini pia amekuwa kiongozi mwanamke wa kwanza na Wa mfano katika Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Tuzo ya pili imepewa waziri wa fedha Mwigulu Nchemba ambayo yeye ana shule ambayo anawalipia vijana 300, na kuwajengea nyumba lakini pia kuwasomesha kwa fedha zake mwenyewe ambapo watakapomaliza elimu anawatafutia ajira.

Lakini pia Gavana wa Jijini Nairobi alitunukiwa tuzo ya kuwa kiongozi Bora na wa kuigwa kwa kuhakikisha Kenya inapata mageuzi makubwa na kubadilika.

Mbali na hayo Helena amesema Tuzo nyingine ni kwa Mohammed Mchengerwa akiwa waziri wa Maliasili na utalii ambapo amefanya kazi kubwa ya kufanya vijana kupenda sana utalii na kuchangia namba kubwa ya vijana kwenda kufanya utalii wa ndani ambao wengine wamewekeza katika utalii.