September 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tuunge mkono, jitihada za Dkt.Samia katika nishati safi ya kupikia,-Kapinga

📌 Amesema ajenda ya nishati ya safi ya kupikia inagusa makundi yote ya wanachi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada, za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kapinga ameyasema hayo Septemba 8, 2024, jijini Dar-es-Salaam wakati wa Tamasha la AZIMIO LA KIZIMKAZI, ambalo limetumika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia likihusisha Mamalishe na Babalishe jijini humo.

“Kiongozi aina ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ana maono ya nishati safi ya kupikia hapatikani mara zote, hatokei mara zote hivyo tuna wajibu wa kumuunga mkono katika ajenda hii ambayo faida zake ni nyingi kiafya, kimazingira, kiuchumi na kijamii,”amesema Kapinga na kuongeza:

“Amesimamia maono yake na kuwafanya Watanzania, Afrika na Duniani kote kusimama pamoja naye katika matumizi ya nishati safi ya kupikia,”.

Ameeleza kuwa, Rais Dkt. Samia anathamini watanzania wote bila kujali hali zao na ndio maana ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia inagusa makundi yote ya Wananchi hivyo nao wana wajibu kumuunga mkono katika kuiletea Tanzania maendeleo.